Na Mwandishi Wetu
SHIRIKISHO la Ndondi Tanzania (BFT) limetangaza mabondia 20 watakaounda
timu za taifa za ndondi zitakazoshiriki mashindano ya Afrika.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa BFT, Makore
Mashaga, mabondia 15 wataunda timu ya ndondi ya wanaume wakati watano wataunda
ile ya wanawake.
Kamati ya Ufundi ndio imeteua mabondia hao chini ya kocha David
Yombayomba akishirikiana na makocha wa timu zote zilizoshiriki mashindano ya
taifa yaliyofanyika hivi karibuni.
Mashindano ya taifa yalimalizika kwenye viwanja vya Tanganyika Packers
Aprili 30 na kushirikisha mikoa michache tofauti na ilivyotarajiwa.
Timu hiyo itakuwa chini ya Kocha Mkuu Mkenya, Benjamin Oyombi, ambapo
itashiriki mashindano ya Afrika Brazzavile, Congo baadae mwezi huu.
Mabondia waliochaguliwa;-
Light Fly: Herman Richard (Ngome)
Fly weight : Ibrahim Aballah (Urafiki) George Costantino (Ngome)
Bantam: Ezra Paulo ( Ngome)
Light: Ismail
Galiatano (Ngome) , King
Lucas (Kigoma)
Lightwelter: Mohamed Juma (Ngome) na Kassim
Seleman (Ngome)
Welter: Said
Ramadhan (JKT) na Haruna
Hussein (JKT)
Middle: Seleman Kidunda
Light Heavy: Yusuph Changarawe
Heavy: Haruna swanga (Ngome)
Super Heavy: Mhina Morris (Ngome) na Alex
Sitta (JKT)
Wakati wanawake ni Sara Andrew ( Ngome), Grace Joseph (JKT), Siwatu
Eliuta (JKT), Sarafina James (JKT) na Aliskunda Jonas (Kigoma).
No comments:
Post a Comment