TURIN, Italia
SHUJAA aliyefunga mabao mawili Gonzalo Higuain amewataka wachezaji
wenzake wa Juventus kugangamala wakati kesho watakaporudiana na Monaco katika
mchezo wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika nchini Ufaransa, Juventus waliibuka
na ushndi wa mabao 2-0, ambayo yalifungwa na Higuain na kuiweka timu hiyo
katika nafasi nzuri ya kutinga fainali.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina alitengenezewa mpira na Dani
Alves na kufunga bao la kuongoza katika dakika ya 29 kabla ya kuihakikishia
ushindi timu hiyo kwa bao la dakika 59 katika mchezo huo uliofanyika kwenye
Uwanja wa Stade Louis II.
Mabingwa hao wa Italia wako katika nafasi nzuri ya kuchea fainali ya
mashindano hayo itakayofanyika kwenye Uwanja wa Cardiff Juni 3 huku
wakitarajiwa kukutana na timu yake yazamani ya Real Madrid.
"Kwa kweli ndoto tuliyokuwa nayo tangu Agosti mwaka jana ni kwenda
Cardiff na tumebakisha hatua moja kuingia, “alisema Higuain, ambaye alipigiwa
makofi na mashabiki huko Monaco.
Kwa sasa tayari ana mabao 31 katika msimu huu kufuatia uhamisho wake
uliogharimu kiasi cha dola za Marekani milioni 98 akitokea Napoli, akiisaidia
Juve kukaribia kutwaa mataji matatu.
Higuain, ambaye alicheza mechi saba bila ya kufunga bao katika Ligi ya
Mabingwa wa Ulaya hatua ya mtoano, aliongeza: "Bado hatujashinda chochote
hadi sasa. Wakati wote niko kimya. Najua kila mmoja ana imani naye.”
Juventus, ambayo itaikaribisha Monaco mjini hapa leo, sasa imecheza saa
10 bila ya kuruhusu bao katika mechi za Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na kipa
Gianluigi "Gigi" Buffon hajafungwa katika mechi zote tano za mtoano
za Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.
"Katika kila mchezo nataka kuonesha kuwea nastahili kucheza katika
kiwango hiki licha ya umri wangu.
Nafanya kazi kwa bidii kila siku hadi pale
nitakapoachia ngazi, “alisema Buffon.
Mara mbili kipa huyo akiwa golini timu yake ilifungwa katika fainali ya
Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.
Buffon pia alimpongeza kocha Massimiliano Allegri kwa uamuzi wake wa
kumleta Andrea Barzagli katika safu ya mabeki watatu, na kuzuia mashambulizi ya
Monaco.
Wakati huohuo, mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya wenyewe
watashuka dimbani kesho Jumatano kucheza na Atlético Madrid baada ya ushindi wa
awali wa mabao 3-0.
No comments:
Post a Comment