Na Mwandishi Wetu, Dodoma
SIMBA ya Dar es Salaam leo imekata tiketi kupanda ndege baada ya
kutwaa taji la Kombe la FA kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbao FC
katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini hapa.
Simba iliandika bao la kwanza katika dakika ya 95 ikiwa ni dakika tano
tangu muda wa nyongeza uanze, lililofungwa na Fredricka Blagnon aliyeingia
akitokea benchi na kuzua shamra shamra kwa wapenzi wa Simba.
Mbao FA walisawazisha bao hilo kupitia kwa Ndaki Robert katika dakika ya
110 baada ya mabeki wa Simba kufikiri kuwa mfungaji ameotea.
Simba walipata penalti katika dakika ya 121 baada ya mchezaji mmoja wa
Mbao FC kuunawa mpira katika eneo la hatari baada ya kutokea piga nikupige na
Shizza Kichuya alifunga penalti hiyo.
Kwa taji hilo, Simba sasa itapata nafasi ya kuliwakilisha taifa katika
mashindano ya Kombe la
Shirikisho Afrika msimu ujao.
Pius Buswuta wa mbao alikosa bao katika dakika ya nne akiwa ndani ya eneo
la hatari, alipiga nje mpira huo.
Simba ilinusurika kufunga mara baada ya kuanza kwa kipindi cha pili
wakati Kichuya akiwa katika nafasi nzuri ya kufunga, alishindwa kufanya hivyo
baada ya Yussuf Ndukumana kuokoa.
Juuko nusura afunge lakini alikosa bao baada ya kupiga kichwa na mpira
kupanguliwa na kipa wa Mbao FA, Benedict Haule.
Nafasi hii inaiwezesha Simba kupanda ndege baada ya kushindwa kufanya
hivyo kwa takribani miaka minne baada ya kuzikosda nafasi mbili za kwanza na
kuwafanya kutoshiriki mashindano ya kimataifa.
Kwa mara ya mwisho Simba ilishiriki mashindano hayo ya kimataifa ni
Februari 17, 2013 walipofungwa mabao 4-0 na DC Libolo ya Angola katika
mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika.
Karibu miaka yote minne, Yanga na Azam ndio walikuwa wakipokezana nafasi
ya kwanza na pili.
Mbao FC pamoja na kucheza mara ya kwanza Ligi Kuu pamoja na fainali hiyo
ya FA, lakini ni timu imara hasa ukizingatia ilizifunga Yanga, Azam FC, Kagera
Sugar na Mtibwa Sugar katika ligi.
Kwa muda mrefu Simba imekuwa ikiitwa wa matopeni huku Yanga ikiwa ya
kimataifa kufuatia timu hiyo kushindwa kufuzu kwa michezo ya kimataifa wakati
watani zao walikuwa wakifuzu kila mwaka na kufanikiwa kupanda ndege.
Vikosi vilikuwa Simba: Daniel Agyei, Jamvier Bukungu, Mohamed Hussein,
Juuko Murshid, James Katei, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Mzamini Yasin, Laudit
Mavugo, Said Ndemla/Fredricka Blagnon na Juma Luizio/Ibrahim Ajibu.
No comments:
Post a Comment