Na Mwandishi Wetu
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga
leo wameshindwa kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo baada ya kulazimishwa
sare ya kufungana bao 1-1 na timu iliyopanda daraja ya African Lyon katika
kipute kilichopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Kabla ya mchezo huo wa leo, Yanga ilikuwa na pointi
36 huku watani zao Simba wakiwa pointi 38, mbili zaidi ya wenzao hao na kama
Vijana hao wa Jangwani wangeshinda mchezo huo wa leo, basi wangekalia kiti cha
uongozi japo kwa muda kabla ya Simba kesho Jumamosi kukutana na JKT Ruvu kwenye
Uwanja huohuo wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Endapo Simba itashinda kesho, basi itafikisha jumla
ya pointi 41 wakati Yanga wakiwa na pointi zao 37, hivyo watakuwa wamepitwa kwa
pointi nne na kuzidi kujiweka katika wakati mgumu wa kutetea taji lao hilo.
Athari
za Mgomo?
Wengi wanajiuliza kama kweli matokeo hayo ya sare
dhidi ya timu iliyopanda daraja ni athari za mgomo wa wachezaji wa timu hiyo
hivi karibuni wakidai fedha zao za mishahara?
Wachezaji wa timu hiyo ndio wanajua siri ya matokeo
ya mchezo huo kama ni matokeo halalai au ni moja ya njia za kuushinikiza
uongozi wa timu hiyo kuwalipa fedha zao katika kipindi hiki cha Sikukuu za
Krismas na Mwaka Mpya.
Yana ilishindwa kupata mabao baada ya kocha wao mpya,
Mzambia George Lwandamina kuljaza viungo watano, Haruna Niyonzima, Simon Msuva,
Thabani Kamusoko, Said Juma na Deus Kaseke akitumia mshambuliaji mmoja tu,
Amissi Tambwe.
Yanga walilisakama lango la Lyon kuanzia dakika ya
tatu baada ya Tambwe kupiga kichwa vizuri akimalizia krosi ya Msuva, lakini
mpira ukaenda juu kidogo na dakika ya 33 Niyonzima akapiga juu ya kuikosesha
timu yake bao la wazi.
Venance aliyesajiliwa dirisha dogo kutoka Mbao FC ya
Mwanza, alifunga bao hilo baada kuingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya
Awadh Juma.
Hata hivyo, bao hilo halikudumu sana, kwani Yanga
walifanikiwa kusawazisha dakika ya 74 kupitia kwa mkali wake mabao, Amissi
Tambwe akimalizia krosi nzuri ya beki wa kulia Juma Abdul.
Wakati
huohuo, ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa Simba kucheza na
JKT Ruvu, huku Mbeya City ikiwa mwenyeji wa Toto Africans ya Mwanza, Stand
United itacheza na Kagera Sugar, Ndanda FC itakwaana na Mtibwa Sugar, Majimaji
dhidi ya Azam FC, Mwadui watakwaana na Mbao FC wakati Ruvu Shooting wenyewe
watacheza Jumatatu dhidi ya Mwadui.
No comments:
Post a Comment