RAIS wa Chama cha Soka cha Afrika Kusini (SAFA)
wakati wa fainali za Kombe la Dunia 2010 nchini humo, amefungiwa kwa miaka
mitano akihusishwa na kupanga matokeo yanayoihusu timu ya taifa ya nchi yake ya
Bafana Bafana,
Uchunguzi wa awali wa Shirikisho la Kimataifa la Soka
(Fifa) ulipata ushahidi kuwa mechi nne za kirafiki za Afrika Kusini kabla ya
fainali hizo za Kombe la Dunia zilizofanyika katika ardhi ya nyumbani matokeo
yake yalipangwa.
Fifa imemkuta na hatia Kirsten Nematandani, aliyeiongoza
Safa kuanzia mwaka 2009-2013,baada ya bosi huyo kushindwa kurioti tuhuma za
rushwa na kutotoa ushirikiana kwa Fifa wakati wa uchunguzi huo.
Alikuwa mmoja wa Waafrika waliofungiwa jana Alhmisi,
pamoja na kiongozi wazamani wa soka za Zimbabwe, Jonathan Musavengana na kocha
wazamani wa Togo, Bana Tchanile.
Wawili hao wamefungiwa maisha kutokana na rushwa
kuhusiana na mechi za kirafiki nchini Afrika Kusini.
Musavengana awali alikuwa akihusishwa na kujihusisha
na kitengo cha kuwahonga wachezaji wa timu ya taifa ya Zimbabwe ili wafungwe wakati
wa ziara ya timu yake Asia mwaka 2009 madai ambayo aliyakanusha.
Wakati huohuo, Tchanile alikuwa tayari ameshafungiwa
kujihusisha na masua la soka kwa miaka mitatu na shirikisho la soka la nchi
yake baada ya kuieleka timu ya Togo kucheza mechi ya kirafiki na Bahrain mwaka 2010.
Moja kati ya mechi za Afrika Kusini ilichezwa siku 11
kabla ya kuanza kwa fainali hizo za Kombe la Dunia za mwaka 2010, ambazo
zilifanyika nchini humo.
Mei 31 huko Polokwane, Bafana Bafana ilisambaratisha Guatemala
5-0 katika mchezo ambao ulikuwa na penalty tatu za utata zilizotolewa na
mwamuzi wa Nigeria.
Fifa inaamini kuwa mechi dhidi ya Thailand, Bulgaria na
Colombia, ambazo pia zilifanyika Mei 2010, matokeo yake yalipangwa.
Katika fainali hizo za Kombe la Dunia mwezi
uliofuata, Afrika Kusini ndio ilikuwa nchi ya kwanza kabisa mwenyeji kushindwa
kufuzu kutoka katika hatua ya makundi.
Oktoba 2015, Fifa ilimfungia kiongozi mwingine
wazamani wa Safa, Lindile Kika – kujihusisha na soka kwa miaka sita.
Shirikisho hilo la soka lilisema hatua hiyo ilikuwa
na uhusiano wa mechi kadhaa za kimataifa za kirafiki zilizochezwa Afrika Kusini
mwaka 2010, madai ambayo aliyakana.
Pamoja na Nematandani, Kika alikuwa mmoja wa maofisa
wa ngazi za juu za Safa waliopewa likizo maalum mwaka 2012 ili kupisha uchunguzi
wa madai ya kupanga matokeo.
No comments:
Post a Comment