LONDON, England
ARSENAL imesisitiza kuwa itafanya kila iwezalo
kuhakikisha inawabakisha kundini washambuliaji wake muhimu, Alexis Sanchez na Mesut
Ozil, anasema kocha wa the Gunners, Arsene
Wenger.
Wachezaji hao amekuwa wakihusishwa na klabu nyingine
na, ikiwa imebaki miezi 18 katika mikataba yao, na wako katika mazungumo ya
kuongeza mikataba mipya na the Gunners.
"Miezi 18 ni mingi katika soka. Wachezaji hawa wamebakisha miezi 18 na
tunawatarajia zaidi, “alisema Wenger.
"Kwa kweli siamini kabisa kama hilo ni tatizo."
Aliongeza kocha huyo: Mkataba ni kati ya pande mbili
na kwa uande wangu nafasi bora ni kufanikiwa hilo mapema.
"Lazima ukubali kuwa makubaliano ni jambo binafsi
na siri na watutakiwi kuelezea nini kinachoendelea katika makubaliano yetu.”
Alipoulizwa kama yuko tayari kuvunja utaratibu wa
mishahara wa klabu ili kuwabakisha wachezaji hao, Wenger alijibu: "Kama
ilivyokawaida tutafanya kila tuwezalo kufanya kile tufanyacho kwa mchezaji
mmoja mmoja.”
Sanchez, ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Chile
amefunga mabao 11 hadi sasa katika Ligi Kuu msimu huu na anaungana na
mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa kwa kufunga mabao mengi msimu huu.
Taarifa za magazeti zinasema kuwa mchezaji huyo
amekuwa akiwindwa na the Blues na klabu moja ya China.
"Kwanini uende China wakati bado unacheza soka
England?” aliuliza Wenger
No comments:
Post a Comment