LONDON, England
KLABU ya Crystal Palace imemtupia virago kocha wao, Alan
Pardew huku klabu hiyo ikikamata nafasi ya 17 katika msimamo wa Ligi Kuu ya
England.
Pardew aliteuliwa kuifundisha timu hiyo miaka mitatau
na nusu iliyopita kuanzia Januari 2015 lakini kocha huyo mwenye umri wa miaka
alijikuta akitupiwa virago baada ya timu yake kushinda mchezo mmoja tu kati ya 11.
Palace imeambulia pointi 26 tu kati ya mechi 36 zilizopita
za Ligi Kuu ya England na iko pointi moja tu juu ya Ukanda wa Kushuka Daraja.
Kocha wazamani wa timu ya taifa ya England Sam
Allardyce ndiye anayepewa nafasi kubwa ya kuchukua mikoba ya kocha huyo.
"Kibinafsi nilikuwa na hisia nzuri kuhusu klabu
hii ya soka na nina huzuni kubwa muda wangu pale umemalizika, “alisema Pardew, ambaye
aliichezea zaidi ya mechi 100 Palace wakati akiwa mchezaji kati ya mwaka 1987 na
1991 na kuiongoza timu hiyo kucheza fainali ya Kombe la FA msimu uliopita,
alisema katika taarifa hiyo.
Mwenyekiti wa klabu hiyo Steve Parish aliongeza:
"Wakati wa kipindi chake cha kuifundisha timu hiyo, Alan alifanya kazi kwa
bidii na alijitahidi kuiimarisha timu hiyo kwa miaka kadhaa.
Hatahivyo, Palace bado haijathibitisha nani atavaa
viatu vya kocha huyo katika mchezo wao wa Ligi Kuu ya Enland utakaofanyika
Boxing Day.
Pardew aliondoka Newcastle na kutua Selhurst Park baada ya Neil Warnock kutimuliwa
na Palace baada ya timu hiyo ikiwa katika ukanda wa kushuka daraja.
Uteuzi wake ulikuwa maarufu kwa mashabiki wakati Palace
ilifanikiwa kukwepoa kushuka daraja kwa kumaliza katika nafasi ya 10, ikiwa ni
nafasi yao bora kabisa kuwa kuipata katika kipindi chao cha kucheza Ligu Kuu ya
Englnad.
Ina maana alikuwa kocha wa kwanza kabisa katika Ligi
Kuu ya England kumaliza katika nusu ya nafasi ya juu baada ya kuwa katika katika
ukanda wa kushuka daraja wakati wa Krismas.
No comments:
Post a Comment