KAMPUNI ya Multichoice Tanzania kupitia king’amuzi
chake cha DStv leo imekabidhi ving’amuzi 24 vya kisasa pamoja na vifurushi vya mwezi mzima kwa
washindi wa shindano la ‘Kapu la Sikukuu’ lililoendeshwa kwa ushirikiano na Kituo
cha Radio cha EFM.
Washindi hao sasa wataweza kusheherekea kwa mbwembwe
Siku Kuu ya Krismas na Mwaka Mpya huku wakiangalia chaneli zaidi ya 70 kupitia
king’amuzi hicho cha DStv ikiwemo michezo mbalimbali pamoja na Ligi Kuu ya
Hispania ya La Liga, Ligi Kuu ya England,
Pia katika kifurushi hicho walichopata kama zawadi
kina chaneli ya Maisha Magic Bongo yenye sinema na tamthilia za Kitanzania
ikiwemo ile maarufu kama ya Huba, ambapo wakongwe wa filamu nchini kama akina
Muhogo Mchungu, Rihami Ali, Mboto, na Hashim Kambi wanaonekana katika tamthilia
hiyo iliyopata umaarufu mkubwa.
Katika hafla hiyo msanii maarufu, Mboto na Irene Paul
ndio waliokabidhi zawadi kwa washindi katika hafla hiyo iliyofanyika leo nje ya
Kituo cha Radio cha EFM Kawe jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi hizo kwa
washindi Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema aliwapongeza EFM kwa jitihada
zao na kuhakikisha wanapata wasikilizaji wengi.
Aidha, Mjema aliwasifu Dstv kwa kutoa zawadi hizo kwa
washindi kwani ni kitu muhimu ambacho pia kitawasaidia kuongeza wateja kwa
kuwashindanisha na washindi kuwapa zawadi katika bahati nasibu iliyoendeshwa na
Kituo cha EFM.
Naye Meneja Masoko wa Multchoice-Tanzania, Alpha Mria
alisema kuwa kampuni yao imeamua kuwatunuku washindi hao ving’amuzi na
vifurushi vya mwezi mzima vya DStv ili kuwawezesha wao na familia zao
kusherehekea vizuri Krismas na Mwaka Mpya majumbani kwao huku wakiangalia DStv.
Mria alisema kuwa Multichoice haijawatunuku washindi
pekee yao, bali na Watanzania wengine ambao wanatumia king’amuzi chao kwani
hivi karibuni walipunguza bei ya vifurushi zao kwa wastani wa asilimia 16, huku
kile kifurushi maarufu zaidi cha DStv Bomba chenye chaneli zaidi ya 70
kikipunguzwa bei hadi kufikia sh. 19,975 tu kwa mwezi.
Baadhi ya washindi waliokabidhiwa zawadi leo ni
pamoja na Kelvin Mhenzi, Asha Said, Dasatan Kaligo, Said Ponela, Grace Kimani,
Leila Ramadhani, Ashura Bakary, Tamirway Kamote, Baraka Mbogoni, Ratipha
Bakari, Gilbert Genese, Luicia John, Ezra Raphael, Nathan William, Caroline
Peter, Seleman Dovya, Alice Sangwani, Mbwana Kuwangaya, Peter Doto, Fadhil
Doto, Fadhil Yusuph, Hadija Hamisi na Mlani Mohamed.
No comments:
Post a Comment