LONDON, England
ARSENAL kesho itashuka dimbani kucheza na West Brom
katika moja ya mechi zitakazopigwa Boxing Day katika kinyang’anyiro cha Ligi
Kuu ya England.
Hatahivyo, timu hiyo huenda ikawakosa baadhi ya
wachezaji wake akiwemo kiungo Aaron Ramsey ingawa alirejea katika mazoezi baada
ya kuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki tatu kutokana na maumivu ya nyama za
paja lakini timu hiyo haiku tayari kujitoa muanga kumchezesha katika mchezo
huo.
Alex Oxlade-Chamberlain naye yuko nje ya uwanja kwa
tatizo kama hilo lakini atarejea katika kipindi cha mwaka mpya.
Mshambuliaji Danny Welbeck, aliyekuwa nje ya uwanja
kwa kipindi cha miezi saba kutokana na maumivu ya goti, amerejea katika mazoezi
kamili ingawa hatachezeshwa katika mchezo huo wa Boxing Day.
Kwa upande wa wapinzani hao wa Arsenal, wenyewe wana
wasiwasi wa kumkosa James Morrison baada ya kukosa mazoezi kutokana na
kusumbuliwa na mafua.
Lakini beki Jonny Evans anaweza kuwemo katika mchezo
huo baada ya kukosa mechi mbili kutokana na maumivu.
BAADA
YA VIPIGO MFULULIZO
Baada ya vipigo mfululizo, Arsenal leo inataka
kujirekebisha na kutoa zawadi ya Krismas kwa wapenzi wake kwa kuibuka na
ushindi katika mchezo huo wa leo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Emirates.
Arsenal ilipokea vipigo mfululizo kutoka kwa Everton na
Manchester City, hivyo wanahitaji kurudisha imani kwa wapenzi wao kwa kuibuka
na ushindi.
"Kwa kiwango cha sasa inawezekana kuwa West Brom
inaweza kumaliza katika nafasi ya juu kuliko katika msimu wowote tangu mwaka 1981.
MAKOCHA WANAUZUNGUMZIAJE MCHEZO
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger: "Hatuko katika
hatari ya kwadharau wapinzani wetu hao. [kocha Tony Pulis] amefanya kazi nzuri
sana.
"Wameimarika vya kutosha. Wamekuwa na
mchanganyiko mzuri kati ya uwezo wao na usuala la ufundi.
"Naamini wanaendeleza uimara wao na kuimarisha
nia yao ya mchezo hasa kwa upande wa
kiufundi.”
Kocha Mkuu wa West Brom, Tony Pulis: "Wakati
wote ni jaribio gumu sana pale tunapokutana na Arsenal. Unatakiwa kuwa katika
kiwango chako bora na itakuwa ni siku ya mapumziko.
"Tunataka mambo yetu yaende kama tunavyotaka.
Wakati fulani wanafanya hivyo.”
UTABIRI
WA MCHEZO HUO
Arsnal inatarajia kurejea katika njia ya ushindi
ingawa inaweza kukumbana na ugumu dhidi ya West Brom, ambayo haijatoa upinzani
wa mara kwa mara msimu huu.
The Baggies ilifungwa na Manchester United wikiendi
iliyopita lakini waliifanya Chelsea kuwa na wakati mgumu wakati walipofungwa tamford
Bridge mapema mwezi huu na watakuwa wakiangalia kurejesha tena kiwango chao, na
kupata matokeo mazuri.
REKODI
ZA TIMU HIZO
West Brom imeifunga
Arsenal mara tatu tu katika mechi 20 timu hizo zilipokutana katika Ligi Kuu ya
England.
Arsenal imepoteza
mchezo mara moja tu kati ya mechi 11 zilizopita dhidi ya West Brom, lakini hizo
ni msimu uliopita wakati Arsenal ilipokuwa mgeni kwenye Uwanja wa Hawthorns,
wakati walipokuwa mbdele kwa bao 1-0 lakini walipoteza kwa 2-1.
Kwa mara ya
mwisho timu hizo zilikutana katika oxing Day ilikuwa mwaka 2002 – ilikuwa Baggies iliyokuwa mbele kwa bao
1-0 kabla ya kupoteza mchezo huo kwa mabao 2-1.
Arsenal haijawahi
kushindwa kufunga walipocheza dhidi ya West Brom katika mechi 20 za Ligi Kuu
timu hizo zilipokutana.
ARSENAL
Baada ya mechi 14 bila ya kufungwa, Arsenal imepoteza
mechi zake mbili zilizopita, ambapo the Gunners ilianza kwa kuongoza kwa 1-0 kabla
ya kupoteza mechi hizo kwa mabao 2-1.
The Gunners haijawahi
kupoteza mechi tatu mfululizo za Ligi Kuu tangu Januari 2012, ambayo pia ni
mara ya mwisho ndio mara yao ya mwisho kupoteza mechi tatu za ligi katika mwezi
mmoja.
WEST BROM
West Brom wenyewe
wamepoteza mechi tatu zilizopita za Ligi Kuu.
Lakini pia waliweza kushinda mechi mbili mwezi huu na
hawajawahi kushinda mechi tatu katika mwezi mmoja tangu Novemba mwaka 2012, Waliposhinda
mara nne.
Unapoangalia rekodi hizo bila shaka Arsenal ina
nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi katika mchezo huo na kutoa zawadi nono ya
Boxing Day kwa mashabiki wake.
No comments:
Post a Comment