Lucas Mhuvile au Joti (mwenye miwani) wakati wa uzinduzi wa msimu wa pili wa vichekesho vya Mwantumu leo katika ofisi za DStv Jijini Dar es Salaam. Kulia ni msanii mkongwe Bafadhili. |
*Sasa Kuonekana Mara Mbili kwa Wiki
*Msimu wa Pili Waja kwa Kishindo Kikubwa
Na Mwandishi Wetu
MSIMU Msimu mpya wa vichekesho maarufu vya Mwantumu ambavyo
huonekana kupitia chaneli ya DStv ya Maisha Magic Bongo, unaanza rasmi Jumanne
Oktoba 16, huku vikiwa vimeongezewa
manjonjo ili kuwahakikishia watazamaji na mashabiki wake burudani isiyo na
upinzani.
Vichekesho hivyo vinavyoongozwa na mchekeshaji
maarufu nchini Lucas Mhuvile maarufu kwa jina la kisanii JOTI ambaye kwenye
vichekesho hivi amevaa uhusika wa watu watatu tofauti.
Joti katikapicha za uhusika tofauti tofauti katika vichekesho vya Mwantumu. |
Joti katika vichekesho hivyo anacheza uhusika wa Mzee Mrisho, Kaboba na
Mwantumu Sahare, ambapo vichekesho hivyo vimekuwa ni moja wa
vipindi vinavyotazamwa sana na kupendwa na maelfu ya watu hapa nchini ambapo
huoneshwa kupitia chaneli maarufu ya Maisha Magic Bongo – DStv 160.
Majina
maarufu pia katika tasnia ya uigizaji na uchekeshaji yatakuwepo msimu huu
akiwemo Mzee Fungafunga (Mzee Mwalubadu), Mama Abduli (Mwantumu Mcharuko), Alex
Wasponga(Kayombo) na wengineo wengi
Shumbana wakati wa uzinduzi wa vichekesho vya Mwantumu leo. |
Amesema msimu huu wa pili, watazamaji wa Maisha Magic
Bongo na mashabiki wa Mwantumu watashuhudia mikasa ya aina yake, ambapo baada ya
Bahati kupata ujauzito, baba yake mzee Mwalubadu anaamua kumpeleka Kaboba
katika vyombo vya sheria kwa kosa la kumpa Bahati ujauzito.
Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania Alpha Mria akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mwantumu leo. |
Hata hivyo suala
hilo linafika kwa Babu yake Kaboba mzee Mrisho, ambaye wakati huohuo hataki
Kaboba apate matatizo yoyote. Kinachotokea hapo ni drama ya aina yake
itakayowaacha watanzamaji wakivunjika mbavu kwa kucheka!
“DStv kupitia Chaneli yake pendwa ya Maisha Magic
Bongo, siku zote imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha tunatoa msisitizo kwenye
maudhui ya ndani na vichekesho hivi ya Mwantumu ni mfano halisi. Hii ni yetu,
imetengenezwa hapa tanzania na wazalishaji, waandaaji na waigizaji wote wa hapa
hapa nchini” alisema Alpha.
Joti akizungumza leo. |
Hii itawapa fursa
mashabiki na watazamaji wa Maisha Magic Bongo kupata burudani zaidi kwani
kumekuwa na maombi mengi ya kuongeza vipindi hivyo kutokana na umaarufu wake.
No comments:
Post a Comment