LONDON, England
KOCHA wa Manchester United Jose Mourinho amempongeza kiungo wake
mpya Paul Pogba baada ya mchezaji huyo ghali zaidi duniani kwa mara ya kwanza
kuanza katika kikosi cha kwanza wakati wakishinda 2-0 dhidi ya Southampton.
Mchezaji huyo aliyesajiliwa kwa ada ya pauni milioni 89 akitokea Juventus alicheza dakika zote 90, ikiwa ni siku 1,616 baada
ya kuichezea timu hiyo mara mwisho.
Alitoa pasi zaidi (71), aligusa mpira (103), alipiga mashuti (4) na
alikabiliana na adui (20) zaidi ya mchezaji mwigine yeyote wa Man United.
Mourinho alisema mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa ameonesha
kiwango cha hali ya juu.
Zlatan Ibrahimovic alifunga mabao yote mawili kwa Man United, na
kufikishamabao matatu katika Ligi Kuu katika mechi mbili. Pia mchezaji huyoa
lifunga katika mchezo wa Ngao ya Hisani.
Baada ya mchezo huo, Mourinho aliulizwa kuhusu Pogba, kiungo
mwenye umri wa miaka 23 aliyeondoka United kwa pauni milioni 1.5 mwaka 2012 na kwenda Juventus, kabla hajarudi tena katika kipindi hiki
cha majira ya joto.
Kwa mara ya kwanza aligusa mpira tangu alipoichezea klabu hiyo
wakati waliposhinda mabao 5-0 dhidi ya Wolves Machi mwaka 2012 ilishuhudia
akifanya kweli.
Kiungo Mfaransa wa Man United Paul Pogba (kulia) akiwa na mwamuzi Anthony
Taylor wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Southampton kwenye
Uwanja wa Old Trafford jana.
|
Mourinho alisema: "Inaonesha uwezo binafsi wa mchezaji.
Mchezo wake wa kwanza na alipogusa kwa mara ya kwanza mpira na kuongoza
mashambulizi ya kushtua na mipira ya adhabu na kuathiri uchezaji wa wapinzani.”
Pogba, ambaye mchezo wake wa mwisho ulikuwa ni ule wa Ufaransa
katika fainali ya Euro 2016 walipofungwa na Ureno, alikimbia sawa na kilometa
11.2, ikiwa ni mchezaji watatu aliyekimbia zaidi ya mchezaji mwingine.
"Alicheza dakika 30 zaidi, anaweza kucheza muda wa nyongeza
bila tatizo, “aliongeza Mourinho.
Pogba alisema: "Ni hisia kubwa. Nilitulia…. Nimekuja hapa kushinda, hicho ndicho ambacho nilikuwa
nakihitaji. Ni klabu kubwa.”
No comments:
Post a Comment