Mwanariadha wa Jamaica, Usain Bolt akivuka mstari na kushika
nafasi ya kwanza.
|
RIO, Brazil
USAIN Bolt alimaliza kazi yake katika Olimpiki baada ya kutwaa
tena medali tatu katika Olimpiki moja na kufikisha medali tisa za dhahabu
wakati Mjamaica huyo aliposhinda fainali za mbio za kupokezana vijiti za meta 4x100
mjini hapa.
Bolt, 29, tayari alikuwa am,eshashinda mbio za meta 100 na 200
hapa na ndiye mtu pekee hadi sasa aliyewahi kushinda mbio zote fupi katika
Olimpiki tatu.
Mwanariadha huyoa naungana na Asafa Powell, Yohan Blake na Nickel
Ashmeade kumaliza kwa kutumia sekunde 37.27.
Japan ilipata medali ya kushangaza ya fedha huku Marekani ushindi
wake watatu ukibatilishwa na kuifanya Canada kutwaa medali ya shaba na
kuisogeza Uingereza hadi katika nafasi ya tano.
'Mwanariadha
mkubwa'
"Kila uendapo. Mimi ni mkubwa," alisema Bolt, baada ya
kumaliza kwa kushangaza historia yake ya Olimpiki katika kipindi chote.
Mwezi Februari, Bolt alithibitisha kuwa atastaafu baada ya
mashindano ya dunia ya riadha yatakayofanyika jijini London mwakani na hatashiriki
katika Michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2020, ambapo atakuwa akikaribia umri wa
miaka 34.
Umwamba wake wa kutwaa medali tisa za dhahabu anaungana kuwa
miongoni mwa wanariadha wakubwa waliowahi kufanya hivyo wakati wengine ni
mkimbiaji wa mbio fupi wa Marekani na mruka chini Carl Lewis na Mfiland
anayekimbia mbio ndefu Paavo Nurmi.
Timu ya Marekani iliyoundwa na Mike Rodgers, Justin Gatlin, Tyson
Gay na Trayvon Bromell ilishangilia ushindi wa medali ya shaba kabla
haijapokonywa.
Timu hiyo ilielezwa kuwa ilipokonywa ushindi huo watatu kwa sababu
Gatlin alipokea kijiti mapema kutoka kwa Rodgers wakati akipokea kwa mara ya
kwanza, lakini wamekata rufaa dhidi ya uamuzi huo.
No comments:
Post a Comment