Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Mawasiliano Tanzania (TTCL) imetoa sh. Milioni
20 ili kudhamini shindano la kumsaka Miss Elimu ya Juu litakalofanyika Oktoba
17 katika ukumbi wa Sigara, Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Warembo wa shindano hilo leo Jumanne wametembelea
Makao Makuu ya TTCL na kushuhudia shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni
hiyo inayomilikiwa na Serikali, ambayo imepania kufanya mambo makubwa katika
sekta ya mawasiliano hapa nchini.
Akizungumza katika ukumbi wa mikutano wa kampuni hiyo
ya mawasiliano muandaa wa shindano hilo, Maya Nkini alisema kuwa jumla ya
warembo 25 kutoka vyuo mbalimbali nchini wako kambini kujiandaa na shindano
hilo, ambalo linatarajia kuwa na ushindani wa hali ya juu sana.
Nkini aliushukuru uongozi wa kampuni hiyo kwa
kudhamini shindano hilo, ambalo sasa litajulikana kama “TTCL Miss Elimu ya Juu 2016”.
Muandaaji wa shindano la Miss Elimu ya Juu nchini,Maya Nkini akizungumza na waandishi wa habari leo. |
Aliwataja wadhamini wengi kuwa ni pamoja na Time,
Darling, AJ Events, ambao pia ndio waandaaji wa shindano hilo wakati wengine ni
Radio E FM, Hussein Pamba Kali na wengine.
Alisema kuwa washindi watatu wa kwanza watakata
tiketi ya kushiriki katika shindano la Miss Tanzania 2016 litakalofanyika
baadae mwaka huu.
Manager Customer Care wa TTCL, Aron Msonga. |
Naye Maneger, Customer Care wa TTCL Aron Msonga
aliwaelezea warembo hao kuhusu shughuli na mikakati ya mizima ya kampuni hiyo
kuhakikisha inarejea kwa kishindo katika sekta ya mawasiliano nchini na tayarri
imefanya mambo kibao.
Mmoja wa waratibu wa Miss Tanzania Makoye alisema
kuwa wamepokea kwa mikono miwili udhamini huo wa TTCL kwa Miss Elimu ya Juu na
kuwaambia kuwa milango iko wazi kwa kampuni hiyo kuingia katika Miss Tanzania.
Warembo wakigawiwa kadi za Simu za TTCL na Manager Cutomer Care, Aron Msonga. |
Alisema kuwa TTCL imeonesha mfano kwa makampuni
mengine kwa kudhamini shindano hilo na wao (Miss Tanzania) hawatawaangusha.
Warembo wote pamoja na viongozi wao waligawiwa line
za simu za 4G zenye muda wa maongezi.
Makoye akiteta na muandaaji wa Miss Vyuo vya Elimu ya Juu, Maya Nkini.
No comments:
Post a Comment