Wanariadha wakianza mchuano katika mbio za nusu Marathon za Kimataifa za Kili FM zilizofanyika Moshi mwishoni mwa wiki. |
Na Mwandishi Wetu, Moshi
HATIMAYE lile tukio lililokuwa likisubiriwa na wakazi
wengi wa mji wa Moshi na maeneo ya jirani, Kili FM International Marathon
limefanyika jana, huku Watanzania na Wakenya wakiwania ufalme wa mbio hizo za kwanza kufanyika na kuvutia mamia ya
washiriki kutoka ndani na nje ya nchi.
Tofauti na miaka ya hivi karibuni ambako Watanzania
wamekuwa wanyonge nyumbani mbele ya Wakenya, jana walikataa kuendeleza uteja na
kupambana vilivyo, hasa katika mbio za kilometa 21, ambapo Gabriel Gerald alitwaa ubingwa kwa upande wa wanaume.
Baadhi ya washiriki wa mbio za kilometa 21 kwa upande wa wanawake wakichuana jirani na mashamba ya miwa ya kiwanda cha Sukari cha TPC Moshi. |
Gabriel Gerald, kijana anayekuja juu hivi sasa hapa
nchini, alipeperusha vema bendera ya Tanzania baada ya kuwapiku Wakenya na
washiriki wengine na kukamata nafasi ya kwa wanaume akitumia saa 1:05.05. Kwa
ushindi huo, alijinyakulia kitita cha sh 700,000 na medali ya dhahabu.
Mkenya Kennedy Kimathi, alimaliza wa pili kwa akitumia
saa 1:05.29 wakati nafasi ya tatu ilikwenda kwa mkonwe Dickson Marwa wa
Tanzania aliyetumia saa 1:05.34.
Washindi wa pili na watatu kila mmoja aliondoka na
zawadi ya sh 500,000 wakati nafasi ya nne ilikwenda kwa mwanariadha wa Kenya,
David Kilimo aliyetumia saa 1:06.02 wakati watano ni Mtanzania, Agustino Sule
aliyetumia saa 1:06.17.
Kwa upande wa wanawake Wakenya walijitutumua na Nancy
Kiprop aliyetumia saa 1:15.00, nafasi ya
pili ikitwaliwa na Mtanzania Magdalena Crispin kutoka Ausha aliyetumia saa
1:15.03 akifuatiwa na mwenzake Failuna Abdi pia Arrusha saa 1:16.0 huku nafasi
ya nne ikichukuliwa na Angelina Tsere 1:16.36 wakati nafasi ya tano ikaenda kwa
ladis Chepoi kutoka Kenya saa 1:17.0.
Wakichuana katika mbio za kilometa tano za kujifurahisha. |
Katika mbio hizo zilizodhaminiwa na Radio Kili FM
chini ya Mkurugenzi wake, Deo Lekule, washindi wa kwanza hadi 20 wote walipata
zawadi na kuwa mbio ya kwanza kulipa washindi wengi.
Kwenye mbio za Km 5 zilitawaliwa na Watanzania ambako
nafasi ya kwanza kwa wasichana ilikwenda kwa Cecilia Ginoka wa Arusha
aliyetumia dakika 19:38.29 akifuatiwa na Amina Mohamed 20:31.94 huku nafasi ya
tatu ikienda kwa Angel John 20:58.2 wote kutoka Arusha.
Nafasi ya nne ilienda kwa mwanariadha wa siku nyingi
Banuelia Brighton wa Kilimanjaro aliyetumia dakika 21:0582 huku mshindi wa tano
akiwa ni Asma Rajab wa Arusha akitumia dakia 21:05.82.
Mshindi wa kwanza wa mbio za kilometa 21 kwa wanawake, Nancy Kiprop akizungumza na waandishi wa habari |
Kwa upande wa wanaume mshindi aliibuka Faraja Thomas
aliyetumia dakika 15:445.15 akifuatiwa na Josephat Joshua 1:47.70 wa tatu
Sylivester Simon 15:49.43 wa nne mkongwe Msenduki Mohamed 15:49.86 hukju nfasi
ya tano ikienda kwa Lukinga James 16:27.70.
Kwa upande wa mbio za watoto Km 2.5 wavulana, mshindi
aliibuka Rashid Naasi wa Police Line Moshi aliyetumia dakika 9:35, wa pili
Japhari Abdul wa Pasua 9:43 wa tatu Loloo Yusuph 10:10:35 kutoka Amani huku wa
nne akiwa ni Nickson Patrick 10:45 wakati wa tano akiibuka ni Mathayo Jiange
dakika 10:54 wote kutoka Amani.
Km 2.5 wasichana mshindi aliibuka Raphia Twalib
kutoka Kikavu dakika 12:03, wa pili Getruda Talalai 12:12 wa Amani, wa tatu
Hadija Alpha wa Majengo 12:17 huku wan ne akiibuka Lulu Shaba wa Mbuyuni 12:22 wakati
nafasi tano ilienda kwa Grace Gastone kutoka Mwereni dakika 12:30.
Akizungumza katika mbio hizo, Kaimu Katibu Mkuu wa
Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Ombeni Zavala, mbali na kuipongeza Kili FM
radia kwa kuamua kuwekeza katika mchezo wa riadha, aliwataka wakazi wa Moshi
kuzidi kushirikiana na waandaaji hao kuendeleza tukio hilo linalochangia kukua
kwa vipaji vya riadha hapa nchini.
Mkurugenzi wa Radio ya Kili FM, Deo Lekule, ambaye pia ndiye muandaa na mdhamini mkuu wa mbio hizo akifuatilia kwa makini wakati wa utoaji wa zawadi baada ya mbio hizo. |
Aidha, Zavala, aliwaonya wakimbiaji kutoka nje ya
nchi kuzingatia kuwa na mialiko maalumu kutoka kwenye mashirikisho yao
wanapokuja hapa nchini, vinginevyo watazuiawa kushiriki.
Naye Mgeni rasmi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Wilbroad Mutafungwa,
aliwapongeza waandaaji na kuahidi mbio zijazo jeshi la polisi litashiriki
kikamilifu na ana uhakika watafanya vizuri.
Nani alisema Wachaga hawana ngoma? Ngoma ya Rosi, ambayo huchezwa wakati wa sherehe za Mangi nayo ilikuwepo kutumbuiza washiriki na watazamaji. |
Alimtaka mwandaaji, kutokuona kama amepoteza kwa
kile alichokifanya bali kina manufaa makubwa kwa jamii ya watu wa Kilimanjaro
na maeneo mbalimbali.
Tukio hilo lilipambwa na burudani mbalimbali ikiwamo
ngoma ya asili ya kichaga ya Rosi na muziki wa kizazi kipya kutoka kwa kundi la
Mamong’oo kutoka Arusha, ambalo liliwakuna wengi.
Mbio hizo mbali na kuendeleza vipaji vya riadha
ilikuwa na kauli mbiu ya mauaji ya walemavu wa ngozi, albino na ujangili, hususan
mauaji ya tembo
No comments:
Post a Comment