Bondia Jonas Junius akiongoza timu ya Namibia katika ufunguzi wa Michezo ya 31 ya Olimpiki jijini hapa Ijumaa iliyopita. |
RIO, Brazil
BONDIA wa Namibia Jonas Junius amekamatwa
kuhusiana na vitendo vya ubakaji katika Kijiji cha Olimpiki, Polisi wa hapa
wamethibitisha hilo.
Junius, ambaye ni bondia wa uzito wa light-welter,
ambaye alikuwa apigane na Hassan Amzile katika raundi ya kwanza kesho Alhamisi,
alishikiliwa baada ya kudaiwa kujaribu kumkumbatia na kumbusu mwanamke mmoja.
Ilidaiwa kuwa tukio hilo lilitokea Jumatatu
usiku na Junius, ambaye ndiye aliyebeba bendera ya taifa ya Namibia wakati wa
ufuguzi wa michezo hiyo Ijumaa usiku, alichukuliwa na kupelekwea katika kituo
cha karibu cha polisi huko Recreio kwa mahojiano zaidi.
Taarifa ya polisi iliyotolewa katika mtandao
ilisema: "Recreio ilisema jana, Agosti 7, kuwa Jonas Junius alikamatwa.
"Jonas alijaribu kunyakulia na kumpiga
busu mwanamke…Tukio hilo
lilitokea katika gholofa ya 11 katika jengo la pili la Kijiji cha Olimpiki.”
Chama cha Kimataifa cha Ngumi (AIBA), chombo
cha ngumi za ridhaa, kina taarifa ya suala hilo.
Msemaji wa AIBA alisema: "AIBA inalichukulia
suala hilo kwa umakini mkubwa kuhusu bondia huyo wa Namibia ambaye alitakiwa
kushindana katika Olimpiki ya Rio 2016.
Endapo atashtakiwa, mthumiwa huyo
atashikiliwa katika gereza la Bangu, ambako Mmorocco Hassan Saada amekuwa
akishikiliwa tangu Ijumaa.
Saada anashtakiwa kwa tuhuma za kujaribu kubaka
wafanya usafi wawili katika Kijiji cha Olimpiki, baada ya kumng’ang’ania mmoja, Jumatano.
No comments:
Post a Comment