Taarifa kwa vyombo vya habari
Tarehe: 30th September, 2016
Utiwaji Saini wa Mkataba na Mwanariadha Alphoce Felix
Simbu
Kampuni ya MultiChoice Tanzania imesaini mkataba wa
mwaka mmoja na mwanariadha Alphonce Felix Simbu aliyeshiriki mashindano ya
Olympic ya Rio 2016 yaliomalizika hivi karibuni huko nchini Brazil na kushika
nafasi ya 5 kati ya wanariadha 157 kwenye mbio za Marathon za wanaume.
Katika Mkataba huu, Kampuni ya Multichoice Tanzania
imemzawadia Alphonce Simbu shilling za Kitanzania 1,000,0000 ambazo atalipwa
kila mwezi kwa kipindi cha mwaka mmoja lengo likiwa ni kumsadia katika
maandalizi yake ya mashindano yajayo ya IAAF WORLD CHAMPIONSHIP yanayotarajiwa
kufanyika mjini London Uingereza August 2017.
Vile vile bwana Alphonce Simbu atapatiwa vifaa
maalumu vya kuumuwezesha kufanya mazoezi yake vyema. Vifaa hivi ni kama vile,
viatu na nguo za mchezo wa Riadha.
Si hivyo tu bali
Kampuni ya MultiChoice itamtengenezea makala yenye kuonyesha matukio
mbalimbili aliyopitia ya Kimichezo na Familia siku za nyuma. Vile vile
watarekodi mazoezi atakayo anafanya akiwa katika kambi ya riadha Chuo cha
Wakala wa Mistu Fiti kilichopo West Kilimanjaro eneo la Ngarenairobi Wilaya ya
Sia Mkoa Kilimanjaro. Makala hii itarushwa kwenye DStv hapo baadae.
Katika Kipindi cha hicho cha mkataba huu Alphonce
Felix Simbu atakuwa Balozi wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania ambapo atashiriki
katika promosheni mbalimbali kutangaza huduma zake.
Alipokuwa akisaini mkataba huo Mkurugenzi Mkuu wa
Multichoice Tanzania Maharage Chande mbele ya Rais wa Riadha Tanzania na mkuu
wa mkoa wa Simiyu Mh. Anthony Mtaka, mwalimu wa wake Alphonce Nd. Francis John
Marcially pamoja na Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania Furaha Samalu,
alisisitiza kuwa “huu ni mwanzo na kadri mafanikio yanavyo ongezeka Multichoice
itakuwa tayari kuwa mstari wa mbele kushirikiana na chama cha riadha Tanzania
katika kunyanyua riadha Tanznaia na kurudisha heshma ya taifa kwenye mchezo
huo”.
Imetolewa na:
Shumbana Walwa|Social Media Administrator
Telephone: +255222199600 Mobile: +255716578662
Email: Shumbana.Walwa@tz.multichoice.com
No comments:
Post a Comment