|
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Nape Nnauye akipokea maelezo mbalimbali kutoka kwa Mhandisi Diana
Munubi jana katika banda la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kwenye
maonesho ya Nanenane Kitaifa mkoani Lindi, kabla ya kufungwa na Makamu wa Rais,
Samia Suluhu Hassan.
|
|
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Nape Nnauye akiwaeleza jambo washiriki wa maonesho ya Nane Nane wa
banda la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), alipotembelea jana kwenye viwanja vya Ngongo
mkoani Lindi. Maonesho hayo yalifungwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu
Hassan.
|
|
Mkuu wa mkoa wa Lindi, Mhe. Geofrey Zambi (wa
kwanza kulia) akipokea maelezo mbalimbali kutoka kwa Mhandisi Diana Munubi (wa
pili kushoto), wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania (TAA), kwenye maonesho ya
Nanenane mkoani Lindi.
|
|
Fatma Matimba (kulia) akitoa maelezo kwa
wanafunzi wa shule ya sekondari ya Lindi, juu ya ufanyaji wa kazi wa kifaa cha
ukaguzi wa abiria kabla ya kuingia eneo la kwenda kupanda ndege, walipotembelea
banda la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), katika maonesho ya
Nane Nane kitaifa Lindi.
|
|
Nuru Nyoni (kulia) akitoa maelezo ya kifaa
cha ukaguzi kwa mkazi wa Lindi, alipotembelea banda la Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege Tanzania (TAA), kwenye maonesho ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja
vya Ngongo mkoani Lindi. |
|
Bahati Mollel (kushoto) akiwafafanulia jambo
wanafunzi wa shule ya sekondari ya Ngongo juu ya viwanja vya ndege vilivyo
chini ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), walipotembelea banda la
mamlaka hiyo katika maonesho ya Nane Nane kitaifa mkoani Lindi. |
Janet Mugini (kushoto) akitoa maelezo
mbalimbali kwa mkazi wa Kilwa, aliyetembelea banda la Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege Tanzania (TAA), kwenye maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa mkoani
Lindi.
|
Edward Kimaro (kulia) akimwelekeza mkazi wa
Lindi namna ndege inavyopaa baada ya kutembelea banda la Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege Tanzania, katika maonesho ya Nanenane kitaifa mkoani Lindi.
|
No comments:
Post a Comment