MOGADISHU, Somali
ASKARI tisa wa Uganda ambao wanafanya kazi kama
walinzi wa amani nchini hapa wamefungwa kwa kupatikana na hatia ya kushiriki
katika mchongo wa kuiba mafuta, imeelezwa.
Taarifa ya Umoja wa Afrika (AU) imesema kuwa askati hao
wamefungwa jela kati ya mwaka mmoja hadi mitatu na mahakama ya Uganda, iliyokaa
nchini Somalia.
Maofisa hao ni pamoja na mameja wawili, walikamatwa
katika zoezi maalum lililofanyika mwezi Juni.
Jeshi hilo la AU linapambana pamoja na Jeshi la Serikali
ya Somalia dhidi ya Jeshi la Kiislamu la al-Shabab.
Hii ni mara ya kwanza kwa mahakama ya kijeshi inayohusiana
na Kamati ta AU (Amisom) kukaa nchini Somalia tangu jeshi hilo liundwe miaka
tisa iliyopita.
Askari hao tisa ni miongoni mwa wale 1 waliosimama
mbele ya mahakama wakidaiwa kuuza mafuta ya Amisom kwa raia katika mji mkuu huo
wa Somalia, Mogadisho, taarifa ya Amisom ilisema.
No comments:
Post a Comment