Msimu Mpya Wa Soka Unakujia Kupitia SuperSport
• Mechi ZOTE 760 za misimu mipya ya Ligi
Kuu Ya Soka Uingereza (Premier League) & Ligi Kuu Ya Soka Hispania (La
Liga) zitapatikana kupitia DStv.
Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice-Tanzania, Maharage Chande akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. Kulia kwa Chande ni Meneja Masoko, Furaha Samalu. |
SuperSport itawaletea watazamaji na
wapenzi wa soka michezo kabambe ya soka kuliko ambavyo imewahi kuonekana
kabla kutoka kwenye UEFA Super Cup, Ligi Ya Mabingwa ya UEFA, Kombe la FA,
Kombe la Capital One, Super Cup ya Hispania, Fainali ya Copa Del Rey, German
Cup na mingine mingi.
August 10, 2016- Msimu mpya ya Ligi bora za soka ulimwenguni
imewadia na kuanzia Jumamosi tarehe 13 Agosti, Ulimwengu wa Mabingwa,
SuperSport, utawaletea mashabiki wa soka barani Afrika michuano yote moja kwa
moja (Live) ya msimu mpya katika kiwango cha HD kupitia DStv!
Baadhi ya waandishi wa habari katika mkutano na Mkurugenzi Mtendaji wa Multchoice-Tanzania, Maharage Chande. |
Mashabiki wa soka mlipatiwa kionjo cha msimu ujao wa soka mwishoni
mwa wiki iliyopita wakati DStv ilipoonyesha pambano lililokuwa linasubiriwa kwa
hamu la kugombea Ngao Ya Hisani ambalo lilishuhudia Man United wakitwaa kikombe
cha kwanza mbele ya mabingwa wa Ligi Kuu Ya Uingereza msimu uliopita, Leicester
City. Na kama shauku na mpagao wa msimu uliopita ni dalili ya chochote, basi
msimu huu mpya wa Ligi Kuu Ya Soka Uingereza utakuwa sio wa kawaida huku mechi
zote 380 zikipatikana kupitia DStv!
Kwa uhakika mechi zisizopungua 300 zitaonyeshwa moja kwa moja
(Live) kitu ambacho kinathibitisha kwamba SuperSport ndio mpango mzima kwa
wapenzi na watazamaji wa soka na matukio mengine ya kimichezo barani Afrika.
Chaneli hii ya michezo hukuletea matangazo kwa mapana na marefu ambayo
hujumuisha uchambuzi wa kina wa Premier League kutoka kwa wachambuzi mahiri wa
soka ambao hawana upinzani kokote barani Afrika.
Msimu huu unaokuja utaleta kivutio kikubwa zaidi huku Premier
League ikiwa na mechi za siku ya Ijumaa kwa mara ya kwanza. Hizi pia zitakuwa
sehemu ya ofa kutoka SuperSport kwenda kwa mashabiki wa soka. Kama kawaida siku
za Jumamosi zitaendelea kuwa za soka kwa mechi zinazoanza saa Kumi Jioni (4pm)
kwa saa za Afrika ya Kati ambapo SuperSport itakuwa inarusha hadi michezo
mitatu ya ziada kwa wakati mmoja kupitia chaneli mbalimbali za SuperSport SS3,
SS5, SS6, SS7 na SS11. Chaneli maarufu
ya Premier League ya masaa 24 itaendelea kuwepo kupitia SS11 kuendelea
kuthibitisha kwamba SuperSport ndio makazi ya soka la kimataifa.
Kwa wapenzi wa soka la Ligi Kuu ya Uingereza, patakuwa na burudani
mfululizo na bila kuchelewa kwani pia kutakuwa na wiki tano ndani ya msimu
ambapo kutakuwa na michezo ya katikati ya wiki ambayo itarushwa katika siku za Jumanne na Jumatano.
Msimu unaanza Jumamosi tarehe 13 Agosti na kumalizika Mei 21,2017.
Lakini Sio Hayo Tu!!
Wateja wa kifurushi cha DStv Compact wataendelea kufurahia soka
kutoka katika ligi kabambe ulimwenguni. SS11 itaendelea kuwa makazi maalum ya
Ligi Kuu Ya Uingereza huku SuperSport 12 ikiwa tena chaneli maalumu ya masaa 24
kwa ajili ya Ligi Kuu Ya Hispania (La Liga) ambapo timu kama Real Madrid na
Barcelona zitakuwa na mengi ya kuvutia pindi msimu mpya utakapoanza tarehe 19
Agosti 2016.
Shukrani kwa muda tofauti wa kuanza kwa mechi za La Liga, asilimia
80% ya mechi 380 zitaonyeshwa Live. Mechi zilizobakia zitaonyeshwa kwenye SS5
au SS7 aidha Live au kwa kuchelewa.
Ligi ya Europa (The Europa League) pia itaonyeshwa kwa matangazo ya mechi zote 205 huku mechi 120 kati ya hizo zikionyeshwa moja kwa moja(Live). Michuano mingine kabambe itakayoonyeshwa kupitia SuperSport ni pamoja na FA Cup, Capital ONE Cup, Spanish Super Cup, Copa Del Rey final na German Cup.
Ili kuhakikisha kwamba wapenzi wa soka wa DStv hawatokosa tukio
lolote, kutakuwa na matangazo kutoka pande zote za dunia kupitia tovuti ya
SuperSport na pia app mpya ya SuperSport, zote ambazo zitakuwa na live
streaming na pia video za yaliyojiri na kuvutia wengi. Huduma maarufu ya DStv
Catch Up iliyopo kwenye DStv Explora pia itakuwa na matukio yaliyojiri kutoka
kwenye mechi zote kubwa.
Isitoshe, matokeo ya mechi zinazoendelea, matokeo na
habari za papo kwa hapo zinaweza kupatikana kupitia tovuti ya supersport.com,
app na simu au vifaa vingine vya viganjani (mobile versions).
Kwa taarifa zaidi kuhusu soka ambalo halipatikani kwingine kokote
zaidi ya DStv na mechi zinazokuja na mengi mengineyo tafadhali tembelea
www.supersport.com
No comments:
Post a Comment