ZURICH, Uswisi
RAIS wazamani wa Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa),
Joao Havelange (pichani), amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 100.
Mbrazil huyo nafasi yake ilichukuliwa na Sepp Blatter
katika chombo hicho cha soka, ambapo alikitumikia kuanzia mwaka 1974 hadi 1998.
Pia alijiuzulu kama rais wa heshima wa Fifa Aprili mwaka
2013 kufuatia uchunguzi kuhusu madai ya rushwa dhidi yake, ambapo mwaka uliofuata alilazwa
hospitalini kutokana na maambikizo katika mapafu.
Wakati wa uhai wake alikuwa mjumbe wa Kamati ya
Utendaji ya Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) kuanzia mwaka 1963 hadi 2011,
alijiuzulu kutokana na matatizo ya kiafya.
"Alikuwa na wazo moja kichwani mwake ni kuufanya
mchezi wa soka kuwa mchezo wa ulimwengu mzima huku kauli mbiu yake ikiwa ‘soka
ni mchezo wa wote’ ,alisma mbadala wake Sepp Blatter.
Havelange aliiwakilisha Brazil katika mchezo wa
kuogelea katika Michezo ya Olimpiki ya 1936, mwaka ambao alifuzu kuwa
mwanasherria, kabla hajachaguliwa IOC.
Akiwa rais wa fifa aliongeza timu zinazoshiriki
fainali za Kombe la Dunia kutoka 16 hadi 32, ambapo fainali sita zolifanyika
chini yake.
Hatahivyo, historia yake ya soka ilichafuliwa na
madai ya rushwa.
Kujitoa kwake katika IOC miaka mitano iliyopita
akiogopa uchunguzi wa madai ya ISL, ambayo Havelange alikanusha tuhuma hizo.
No comments:
Post a Comment