LONDON, England
KLABU ya Arsenal iko katika mazungumzo na FC Basel kuhusu
kumsajili kiungo wa kati Mohamed Elneny (pichani).
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri mwenye umri wa miaka 23
alijiunga na klabu hiyo yenye maskani yake Uswisi mwaka 2013 na ametwaa mataji
ya ligi katika kila msimu alioichezea timu hiyo.
Kiasi cha ada kilichoelezwa ni kama pauni milioni 5 na Elneny anahitaji kibali cha kufanyia kazi ili kuichezea timu hiyo.
Mchezajji huyo ruksa kuichezea Arsenal katika michuano ya Ligi ya
Mabingwa wa Ulaya baada ya Basel kushindwa kufuzu mwaka huu katika hatua ya
makundi.
Elneny alikuwemo katika kikosi cha Basel kilichoibuka na ushindi
dhidi ya Chelsea katika mashindano ya msimu wa mwaka 2013-14.
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger yuko mbioni kuimarisha kikosi chake
hasa katika nafasi ya kiungo wa kati baada ya Francis Coquelin na Santi Cazorla
kupata majeraha makubwa, huku Aaron Ramsey na Mikel Arteta nao pia wako nje ya
uwanja na Jack Wilshere bado hajarejea uwanjani.
Hatahivyo, Elneny anaonekana kama sehemu ya mpango ya muda mrefu wa
Wenger na sio kuziba pengo, wakati atakapojiunga na klabu hiyo yenye maskani
yake kaskazini ya London.
Wilshere atakuwa nje ya uwanja angalau hadi mwezi Februari.
Kocha huyo wa the Gunners alikiri kuwa, hana uhakika kama Wilshere
atarejea haraka uwanjani, lakini sio kabla ya Februari.
Kiungo huyo wa England alitarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa angalau
miezi mitatu baada ya kufanyiwa upasuaji Septemba baada ya kuumia katika mguu
wa kulia, lakini makadilio hayo yameongezeka.
"Nilisema Februari lakini ukweli sina uhakika,” alisema Wenger wakati timu yake
ilipochezea kichapo cha mabao 4-0 katika Ligi Kuu ya England kutoka kwa Southampton
huku leo Jumatatu timu hiyo ikitarajiwa kuwa mwenyeji wa Bournemouth.
No comments:
Post a Comment