Kocha Mkuu wa Man United, Louis van Gaal (kushotot) akiangalia timu yake ikitoka suluhu na Chelsea pamoja na msaidizi wake, yan Giggs. |
LONDON, England
KOCHA wa Manchester United, Louis van Gaal anasema kuwa kamwe
hatajiuzulu licha ya kushuhudia timu yake ikiteleza hadi nje ya nne bora katika
msimamo wa Ligi Kuu ya England.
Suluhu ya Jumatatu nyumbani dhidi ya helsea ina maana kuwa, Man
United sasa imeshindwa kuibuka na ushindi katika mechi nane katika mashindano
yote.
Hiyo haijawahi kuwatokea tangu mwaka 1990 na kuiacha klabu hiyo
ikiwa pointi tano nyuma ya wapinzani wao wa jiji Manchester City ambao wako
katika nafasi ya nne katika msimamo huo.
Lakini bado Van Gaal alikuwa na moyo na kusema: "Wakati
wachezaji wanaonesha kiwango kama kile pamoja na shinikiza kibao, kwa kweli
hakuna sababu ya kuachia ngazi.”
'Wachezaji
wako Tayari Kupambana'
Siku chache zilizopita kocha, ambaye alianza kuifundisha Man
United tangu Julai mwaka jana, alikuwa majaribuni.
Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 64 aliibuka kabla ya Krismas
baada ya vyomo vua habari kukosoa nafasi yake.
Baadae timu yake ilipokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Stoke, kipigo
kilichoongeza shinikizo la kutimuliwa huku ikidaiwa kuwa nafasi yake inaweza
kuchukuliwa na Jose Mourinho, aliyetimuliwa na Chelsea Desemba 17.
Kabla ya mchezo huo wa Jumatatu dhidi ya the Blues, baadhi ya
mashabiki walikuwa wamebeba skafu zenye jina la Mourinho, ambazo zilikuwa
zinauzwa nje ya Uwanja wa Old Trafford.
No comments:
Post a Comment