Na Mwandishi Wetu,Zanzibar
MABINGWA wa Tanzania Bara Yanga na washindi wa pili Azam FC wako
katika kundi moja la michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa mujibu wa ratiba
iliyotolewa leo na waandaaji wake.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, mashindano hayo yanatarajia kuanza
kutimua vumbi kuanzia Jumamosi, Januari 2 kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.
Kwa mujibu wa Kamati ya Michuano hiyo, jumla ya jumla ya timu nane
zinatarajia kushiriki na zumepangwa katika makundi mawili, huku mabingwa watetezi
Simba wakipangwa kufungua dimba na Jamhuri ya Pemba.
Ratiba hiyo inaonesha kuwa, kabla ya mchezo huo wa ufunguzi, jioni kutakuwa na mchezo
utakaozikutanisha timu za Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) dhidi ya Watoza Ushuru
wa Uganda (URA).
Simba katika mchezo huo imepangwa katika Kundi A pamoja na timu za
JKU, URA na Jamhuri.
Kwa upande wa mahasimu wao Yanga, wenyewe wako katika Kundi B pamoja
na timu za Mtibwa Sugar ya Turiani, Morogoro, Azam FC na Mafunzo.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Sharifa Khamis ametaja viingilio vya
michezo hiyo kuwa ni Sh. 10,000,5,000,
3000 wakati Urusi ni Sh. 2,000 tu.
Simba walitwaa taji hilo mwaka jana kwenye Uwanja wa Amaan baada ya kuichapa Azam FC.
No comments:
Post a Comment