LONDON, England
KOCHA Jose Mourinho anajaribu kuzuia vishawishi vya kurejea haraka
katika klabu yake ya zamani ya Real Madrid wakati akisikilizia hali
inavyoendelea katika klabu ya Manchester United na kwingineko Ulaya kabla
hajafanya maamuzi ya mwisho kuhusu kibarua chake kijacho.
Madrid, ambako Mourinho aliondoka mwaka 2013 na kurudi Chelsea,
wameonesha nia ya kumrejesha kocha wao huyo wazamani kuchukua nafasi ya
mpinzani wake wazamani Rafa Benitez.
Lakini Mourinho kwa sasa anaonekana kama hana mpango wa kurejea Madrid.
Pia familia ya Mourinho, mkewe Tami,
mtoto wake wa kike Matilde na yule wa kiume Jose junior hawana hamu ya
kurejea katika jiji hilo la Hispania,ambalo walikaa kwa zaidi ya mismu mitatu.
Kingine kinachomfanya kocha huyo Mreno kutokuwa na hamu ya kurejea
Madrid ni ile hali ya kutoelewana na baadhi ya wachezaji lakini tangu atimuliwe
na Chelsea, amekuwa katika mipango ta Madrid.
Kwa sasa iko katika nafasi ya tatu, ambapo Jumatano watacheza na Real
Sociedad na Valencia ya Gary Neville wayakwaana nayo Jumapili kabla ya kuanza
kwa mapumziko ya majira ya baridi.
Timu hiyo ilifunga mabao 10
walipocheza dhidi ya Rayo Vallecano katika
mchezo wao wa mwisho wa Ligi Kuu ya Hispania ya La Liga, na kufuatia na kipigo
kutoka kwa Villarreal.
Kwa sasa, Mourinho anasubiri kuangalia mwenendo wa rafiki yake na
bosi wake wazamani Louis van Gaal Man United, ambao leo waikabili Chelsea
kwenye Uwanja wa Old Trafford.
Kocha huyo Mreno alitumia wiki kadhaa zilizopita akivua samaki na
marafiki zake katika pwani jirani na Setubal. Sasa amekwenda Ureno kwa ajili ya
mapumziko na familia yake.
No comments:
Post a Comment