KOCHA WA Chelsea Jose Mourinho anaamini kuwa wapinzani wao katika
Ligi ya Mabingwa wa Ulaya kila moja anataka apanwe na timu yake katika hatua ya
16 bora.
The Blues wamemaliza washindi wa Kungi G baada ya jana usiku
kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Porto, ikiwa na maana kuwa
wanatarajiwa kupangwa dhidi ya moja ya timu sita zilizomaliza katika nafasi ya
pili katika makundi yao
Ratiba hiyo ya hatua ya 16 itapanwa Jumatatu.
Chelsea inaweza kupanwa ama na Paris St-Germain, Juventus, PSV
Eindhoven, Benfica, Roma au Gent.
"Kila timu iliyomaliza katika nafasi ya pili inataka kucheza
na sisi (Chelsea) au Zenit St Petersburg," alisema Mourinho mwenye umri wa
miaka 52.
Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England wamekuwa na wakati mgumu
katika ligi hiyo ya nyumbani ambapo wamepoteza mechi nane kati ya 15
walizocheza katika ligi hiyo msimu huu na kujikuta wakiwa katika nafasi ya 14.
Lakini timu hiyo imekuwa ikifanya vizuri katika mashindano ya
Ulaya ambapo imeshinda mechi nne na kutoka sare moja katika mechi zao sita za
hatua ya makundi na kutina hatua ya mtoano ya michuano hiyo.
The Blues walikata tiketi ya kucheza hatua hiyo ya 16 bora kupitia
kwa Ivan Marcano aliyejifunga katika kipindi cha kwanza huku bao safi la Willian
akilifunga baada ya mapumziko.
"Kila timu inaogopa kucheza na Barcelona, hawataki kucheza na
Real Madrid, hawataki kucheza na Atletico, hawapendi kusikia wanapanwa kucheza
na Bayern Munich," aliongeza Mourinho.
Mourinho ana nia ya kuwa kocha wa kwanza kutwaa mara tatu taji la
Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na klabu tatu tofauti, ambapo aliziongoza Porto na Inter
Milan kutwaa taji hilo mwaka 2004 na 2010.
Na kocha huyo Mreno anasema Blues, licha ya kufanya ibaya katika
ligi ya nyumbani, inaweza kuwazishangaza zile timu zinazopewa nafasi kubwa ya
kutwaa ubingwa.
"Timu ambayo inachechemea ni wazi sio mshindani katika mbio a
ubingwa kwa sababu kuna timu bora zaidi Ulaya “alisema ourinho, ambaye aliwahi pia kuiongoza Real Madrid kati ya
mwaka 2010 na 2013.
"Lakini hata tulipotwaa taji na Porto hatukuwa washindani. Na
hata tulishinda na Inter Milan hatukuwa washindani wa taji hilo.
"Wakati tulipokuwa washindani tuliwa na Real Madrid tulishindwa
katika robo fainali, na tulipoteza nusu fainali mbili na Chelsea.
Muhimu: Timu nane
zilizoshikamnafasi ya kwanza katika makundi yao zinapanwa na nane zilizoshika
nafasi ya pili, inawa timu kutoka nchi moja kamwe haziwezi kupanwa pamoja
katika hatua hiyo ya 16 bora,
Pia timu zilizowahi kukutana katika hatua ya makundi haziwezi
kupanwa pamoja katika hatua hiyo inayofuata.
Kutokana na utaratibu huo inamaana kuwa Chelsea haiwezi kucheza
dhidi ya Arsenal au Dynamo Kiev katika hatua hiyo ya 16 bora.
TIMU ZILIZOFUZU
KWA 16 BORA:
Real Madrid, Paris St-Germain, Wolfsburg, PSV Eindhoven,
Atletico Madrid, Benfica,Manchester City, Juventus,Barcelona,
Roma, Bayern Munich, Arsenal, Chelsea, Dynamo Kiev, Zenit St Petersburg na Gent.
No comments:
Post a Comment