TANZANIA OLYMPIC
COMMITTEE (TOC)
KAMATI YA OLIMPIKI
TANZANIA
PONGEZI/SHUKRANI ZA TOC KWA
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA
KUENDELEZA MICHEZO KATIKA MIAKA 10 YA UONGOZI WAKE
Napenda kuchukua
nafasi hii kuushukuru uongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania
(TASWA) kwa kuandaa hafla ya kutoa tuzo kwa wanamichezo 10 bora waliofanya
vizuri kwa kuiletea heshima nchi yetu
katika miaka 10 ya uongozi wa mwanamichezo mwenzetu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Pamoja na kutoa tuzo
kwa Wanamichezo bora waliofanya vizuri miaka 10 iliyopita, vile vile TASWA ilimtunuku tuzo Mhe Jakaya
Mrisho Kikwete kwa mchango wako katika michezo.
Mhe. Rais, wakati
anazungumza na wanamichezo waliokusanyika katika ukumbi wa Mlimani hapo tarehe
12/10/2015 alisononeka kwa wanamichezo wa Tanzania kutofanya vizuri wakati wa
miaka 10 ya uongozi wake pamoja na kuleta walimu katika baadhi ya vyama vya
michezo.
Mafanikio hata
katika maisha ya kawaida ni mapambano hali kadhalika hata kupata mafanikio
katika michezo ni mapambano. Katika miaka ya 70-80 michezo ilikuwa ridhaa,
lakini kuanzia miaka ya 90 hadi sasa michezo imekuwa biashara na ajira kubwa
kwa wanamichezo.
Kwa mfumo huo wa
michezo kuwa biashara na ajira kila moja angefikiria kwamba tungepaswa kuwa na
wanamichezo wengi kwa hiari yao
kuchangamkia mazoezi ya hali ya juu ili nao waweze kuwa wawakilishi wazuri wa
nchi yetu na kujipatia zawadi nono za fedha, lakini badala yake hali inazidi
kuwa mbaya.
Hali hii inawezekana
vile vile imesababishwa na hali ya ukata wa vyama vya michezo ambao hawana
uwezo wa kutafuta vipaji huko walipo hasa Vijijini, Wilayani na Mikoani. Katika
miaka ya 70-80, Vyama vyetu vilikuwa
vinapata ruzuku kutoka Serikalini kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT),
ruzuku ambayo ilikuwa inawasaidia kuendesha ofisi na kuandaa Mashindano kama ya Taifa ambayo wanamichezo wengi
wanakusanyika na vyama husika kufanya uteuzi wa wachezaji bora wenye vipaji
ambao huwaendeleza. Huo mfumo kwa sasa haupo kutokana na hali inayotamkwa na
vyama vya michezo kama ukata na Serikali (BMT) kutokuwa na fedha.
Katika risala yake
wakati wa tuzo kwa wanamichezo bora, Mhe. Rais alikiri bila kuwekeza tusitegemee
kupata mafanikio, lakini nani awekeze, kwa haraka kwa tulio na uelewa mdogo ni
Serikali ndiyo iwekeze kama nchi zingine duniani inavyofanya.
Mhe. Rais amefanya mengi
kuinua michezo wakati wa uongozi wake. Naomba nitaje chache:
1.
WALIMU WA MICHEZO KUTOKA NJE
Aliweza kuwalipa
mishahara walimu wa michezo kama mpira
wa miguu, netiboli, ngumi na riadha(pamoja
na walimu wa riadha kutokuwa wa viwango) kupitia mpago wa ushirikiano kati ya
Tanzania na Cuba. Kila moja wetu aliona jitihada zake, na nakiri kwamba kwa namna moja au nyingine, vyama/mashirikisho
ya michezo hawakutekeleza wajibu wao kutokana na hali ya ukata. Hata
wanamichezo wetu hawakutambua na kuona michezo kama ajira.
Mhe. Rais anakiri mafanikio
yana gharama, bila nchi kuwekeza hafikirii kama tutakuwa na mwelekeo mwema hasa
kwa vijana wetu kufanya vizuri katika medani ya Kimataifa. Nchi nyingi
zinazofanya vizuri katika michezo ya kimataifa
kwa asilimia kubwa wamewekeza katika michezo. Pamoja na WHVUM kutengewa
bajeti ndogo ya michezo, bado suala la kuwekeza haliwezi kukwepeka kwa hali ya
sasa ya michezo duniani.
Tutakukumbuka hasa
pale Mhe Jakaya aliporejesha michezo ya Umitashumta na Umisseta mwaka 2007 baada ya kusimama kwa zaidi ya
miaka 9.
Binafsi naamini
kilichotufikisha hapa tulipo leo ni pamoja na kutofundishwa kwa elimu ya viungo
(PE) sambamba na kutokwepo walimu wa masomo hayo kwenye shule zetu na kusimama
kwa michezo hiyo na Michezo ya Majeshi (BAMATA).
Michezo ya
Umitashumta/Umisseta ndiyo ilikuwa kiwanda cha kuandaa wachezaji ambapo
wanapofanya vizuri hupata ajira katika taasisi za Serikali (JWTZ, Polisi, Magereza, Jeshi la KujengaTaifa) lakini kwa sasa
imekuwa tofauti kwani taasisi hizo haziajiri kama ilivyo huko nyuma kutokana na
kutofanyika Michezo ya Majeshi (BAMATA) ambayo ilikuwa na ushindani mkubwa.
Ni zaidi ya miaka 8
tangu aliporejesha michezo ya Umitashumta/Umisseta kwa nia na madhumuni yakupata
vipaji vitakavyoendelezwa na kuwa na nafasi nzuri ya kutuwakilisha Kimataifa.
Imekuwa vigumu kuendeleza vipaji
vinavyoonekana katika michezo hiyo kwani hakuna maandalizi yaliyofanywa
kuwaendeleza baada ya michezo hiyo
kumalizika. Hata wale wanaomaliza masomo yao katika ngazi husika hawapati ajira
kutokana na taasisi za Serikali nilizotaja kutokuwa na ajira rasmi kama ilivyo
zamani. Mpaka sasa nishule chache za binafsi
na taasisi zimekuwa na mpango wa
kuwasajili katika shule zao wanafunzi wazuri wenye vipaji na baadhi yao kutoa
elimu bure (Scholarships) na kuwaendeleza katika baadhi ya michezo:
a. Shule ya Sekondari ya Alliance, Mwanza (Mpira wa Miguu na Riadha).
b. Shule za Filbert Bayi, Mkuza, Kibaha Mkoa wa Pwani (Riadha na Netiboli)
c. Shule ya Sekondari ya Lord Baden Powel, Bagamoyo (Mpira wa Miguu kwa Wanaume na Wanawake,
Mpira wa Kikapu, Mpira wa Wavu na Riadha).
d. Shule ya Sekondari ya Winning Spirit,Arusha (Riadha)
e.
Shule ya Sekondari ya Makongo, Dar Es Salaam (Mpira wa Miguu, Netiboli Kikapu na Wavu).
Naomba niishauri
Serikali (Wizara ya Elimu na Tamisemi) kuunda Kanda ili kila baada ya michezo
ya Umitashumta na Umisseta wanamichezo wenye vipaji wawekwe katika shule zilizo
katika Kanda zitakazoundwa wakiendelea na masomo hali kadhalika na kucheza kwa
Wizara husika kupeleka wataalamu (coaches) katika Kanda husika. Kama hilo
haliwezekani, basi shule binafsi na taasisi zisaidiwe ili ziweze kuimarisha
zaidi mipango waliyonayo ya kuendeleza michezo
Bila kuwa na
utaratibu na mipango mahsusi, michezo ya Umitashumta na Umisseta, itakuwa kama tamasha tu.
Hakuna ubishi kwa
ushiriki wake katika ujenzi wa uwanja wa Taifa wakati wa uongozi wa Rais wa
awamu ya tatu Mhe. Benjamin William Mkapa akiwa kama Waziri wa Mambo ya nchi za
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mpaka alipochaguliwa kuwa Rais wa awamu ya nne
na kumalizia kazi za ujenzi zilizobaki.
Uwanja wetu ni mzuri
sana, lakini matumizi yake kwa mchezo wa riadha yamekuwa nadra sana kutokana na
gharama kubwa ambayo wakati mwingine
Riadha Tanzania inashindwa kuchangia hasa inapotaka kufanya michezo ya
Taifa ambayo hufanyika mara moja kwa mwaka.
4.
MAFANIKIO YA MICHEZO WAKATI WA UONGOZI WAKO.
Mhe.Jakata wakati wa
uongozi wake wa miaka 10 kulikuwa na mafanikio ambayo hayaridhishi kwa nchi
kama Tanzania yenye watu zaidi ya Milion 45, lakini kutokana na hali halisi
niliyotaja hapo juu naomba nitaje mafanikio hayo kama ifuatavyo:
1. Samson Ramadhani NYONYI, (Riadha):”Marathon”>Dhahabu: Michezo ya Jumuiya ya Madola, Melbourne, Australia 2006
2. Fabian Joseph NAASI, (Riadha): Mita 10000>Shaba: Michezo ya Jumuiya ya Modola, Melbourne, Australia 2006
3. Martin SULLE, (Riadha) Km 21.1>Medali ya Fedha>Michezo ya Afrika, Algiers, Algeria, 2007
4. Timu ya Netiboli, (Netiboli)>Medali ya Fedha>Michezo ya Afrika, Maputo, Msumbiji, 2011
5. Timu ya Netiboli (Netiboli)>Kushinda Kombe la Mataifa 6, Singapore, 2012
6. Timu ya Netiboli (Netiboli>Nafasi ya Pili, Mashindano ya Africa, Dar Es Salaam, 2012
7. Timu ya Mpira wa Miguu watoto wa Mitaani (Street Children World Cup)>Dhahabu, Mashindano Kombe la Dunia, Rio de Jeneiro, Brazil, 2014
8. Timu ya Mpira wa Miguu-Vijana chini ya Miaka 15>Medali ya Fedha> Michezo ya Vijana Afrika, Gaborone, Botswana, 2014.
Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Gulam Rashid akifungua mkutano mkuu Zanzibar Desemba 12 mwaka huu. Kushoto ni Katibu Mkuu Filbert Bayi na Mhazini Mkuu Charles Nyange. |
Wakati wa uongozi wake wa miaka 10 kama Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kamati ya Olimpiki Tanzania imeweza kufanya
shughuli mbalimbali za maendeleo kwa vyama vya michezo, baadhi ya hizo shughuli
zilikuwa ni kuendesha mafunzo ya ufundi kwa walimu wa michezo kutoka
Vyama/Mashirikisho ya michezo wanachama wa TOC kwa kuleta Wakufunzi kutoka nje
ya nchi hali kadhalika na Mafunzo ya Utawala na Uongozi wa Michezo kwa viongozi
wa Vyama/Mashirikisho ya Mikoa na Taifa kwa nyakati tofauti.
Kwa ujumla Walimu 523
(448/75) na viongozi 380 (304/76)
waliweza kupata elimu ya kufundisha wachezaji kwa madaraja tofauti na uongozi
na utawala bora.
(Orodha
Nyongeza “A” na “B”imeambatanishwa).
HITIMISHO
Kwa niaba ya Kamati ya Olimpiki Tanzania na kwa niaba
yangu napenda nichukue nafasi hii kumshukuru Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo kwa kutoa posho za kujikimu, mavazi ya taifa, vifaa vya mazoezi na
mashindano timu zetu za Taifa zilizowahi kushiriki Michezo ya Jumuiya ya Madola
(Melbourne, Australia 2006, New Delhi, India 2010 na Glasgow, Scotland 2014) na
Olimpiki (Beijing, China 2008, London, Uingereza 2012).
Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitamshukuru Mhe.
Bernard Camillius Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa
ushirikiano na WHVUM kuwatafutia mazoezi ya nje (China, Ethiopia, Uturuki na
New Zealand) kwa kutumia mpango wa Diplomasia ya Michezo (Sports Diplomacy)
wanamichezo wetu kabla ya Michezo ya Jumuiya ya Madola, yaliyofanyika Glasgow,
Scotland mwaka jana (2014).
Akiwa kama mwanamichezo nambari moja hata baada ya
kustaafu bado wanamichezo wenzako tutahitaji ushauri wake katika maendeleo ya
michezo katika
nchi yetu.
Mwisho kabisa napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza
Rais wa awamu ya tano (5) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe
Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu kwa kuchaguliwa kwa kishindo wakati
wa Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, 2015, Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa na
Mawaziri wote kwa kuteuliwa kuongoza nchi yetu kwa miaka tano (5) ijayo kwa
misingi ya “Hapa Kazi Tu”
Ni matumaini yetu wanamichezo kwamba viongozi hao
wataitendea haki michezo kuanzia ngazi ya mashule hadi Kimataifa kwa viongozi
watendaji kuwa makini (serious) kwenye maeneo yao.
Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi. Kulia ni rais Gulam Rashid na mhazini msaidizi, Zaidi. |
Nawatakia Wanamichezo wote kila la kheri kwa mwaka
2016.
Filbert Bayi
KATIBU MKUU
NYONGEZA “A”
TANZANIA OLYMPIC COMMITTEE (TOC)
1.
MAFUNZO YA WALIMU WA MICHEZO
2006-2015
NA.
|
TAREHE
|
CHAMA/SHIRIKISHO
|
MAHALI
|
JINSIA
|
JUMLA
|
|
MME
|
MKE
|
|||||
1.
|
APR.,
2006
|
MPIRA
WA WAVU
|
TANGA
|
25
|
5
|
30
|
2.
|
AUG.
2006
|
TAEKWENDO
|
ARUSHA
|
30
|
4
|
34
|
3.
|
APR. 2007
|
MIELEKA
|
MOROGORO
|
21
|
3
|
24
|
4.
|
SEPT.
2007
|
MPIRA
WA MIGUU
|
ZANZIBAR
|
25
|
-
|
25
|
5.
|
MEI.
2008
|
KUOGELEA
|
DAR
ES SALAAM
|
25
|
5
|
30
|
6.
|
NOV-DEC.
2008
|
MPIRA
WA MIKONO
|
DAR
ES SALAAM
|
27
|
3
|
30
|
7.
|
MEI. 2009
|
TENISI
|
DAR
ES SALAAM
|
21
|
-
|
21
|
8.
|
MAR.
2010
|
BAISKELI
|
ARUSHA
|
25
|
2
|
27
|
9.
|
NOV. 2010
|
RIADHA
|
DAR
ES SALAAM
|
19
|
4
|
23
|
10.
|
JUL. 2011
|
MPIRA
WA MEZA
|
DAR
ES SALAAM
|
16
|
5
|
21
|
11.
|
NOV. 2011
|
JUDO
|
KIBAHA
|
32
|
-
|
32
|
12.
|
JAN. 2012
|
NGUMI
|
KIBAHA
|
23
|
2
|
25
|
13.
|
MEI. 2012
|
MPIRA
WA MAGONGO
|
TANGA
|
20
|
2
|
22
|
14.
|
AUG. 2012
|
MPIRA
WA KIKAPU
|
MOROGORO
|
18
|
11
|
29
|
15.
|
MEI. 2013
|
MPIRA
WA WAVU
|
TANGA
|
27
|
8
|
35
|
16.
|
JUN-JUL.
2014
|
TAEKWENDO
|
ARUSHA
|
28
|
1
|
29
|
17.
|
OKT. 2014
|
MPIRA
WA MIGUU
|
DAR
ES SALAAM
|
29
|
3
|
32
|
18.
|
JUL-AUG.
2015
|
MPIRA
WA MIKONO
|
KIBAHA
|
17
|
10
|
27
|
19.
|
AUG.
2015
|
MIELEKA
|
KIBAHA
|
20
|
7
|
27
|
JUMLA
|
448
|
75
|
523
|
Mwanariadha wazamani wa kimataifa wa Tanzania, Mwinga Mwanjala (kulia), akitoa mafunzo ya kutupa tufe kwa walimu wa shule za msingi nchini. Mafunzo hayo yalifanyika jjijini Dar es Salaam. |
TANZANIA OLYMPIC COMMITTEE (TOC)
KAMATI YA OLIMPIKI TANZANIA
1. MAFUNZO YA UONGOZI NA UTAWALA WA
MICHEZO 2006-2015
NA.
|
TAREHE
|
CHAMA/SHIRIKISHO
|
JINSIA
|
JUMLA
|
||
MKOA
|
TAIFA
|
MME
|
MKE
|
|||
1
|
JAN.
2006
|
MOROGORO
|
19
|
4
|
23
|
|
2
|
MEI.
2006
|
DAR
ES SALAAM
|
19
|
5
|
24
|
|
3
|
JUN.
2006
|
SONGEA
|
19
|
2
|
21
|
|
4
|
JUN.
2007
|
ZANZIBAR
|
20
|
3
|
23
|
|
5
|
JUL. 2007
|
DAR
ES SALAAM
|
13
|
2
|
15
|
|
6
|
MEI.
2009
|
DAR
ES SALAAM
|
17
|
5
|
22
|
|
7
|
OKT.
2009
|
ZANZIBAR
|
22
|
8
|
30
|
|
8
|
JUL. 2010
|
DAR
ES SALAAM
|
17
|
6
|
23
|
|
9
|
AUG-SEPT.
2010
|
ZANZIBAR
|
25
|
5
|
30
|
|
10
|
AUG.
2012
|
ARUSHA
|
23
|
5
|
28
|
|
11
|
JUN.
2013
|
MBEYA
|
30
|
8
|
38
|
|
12
|
OKT.
2013
|
PEMBA
|
25
|
5
|
30
|
|
13
|
OKT.
2014
|
KILIMANJARO
|
14
|
6
|
20
|
|
14
|
NOV.
2014
|
ZANZIBAR
|
26
|
4
|
30
|
|
15
|
JUN. 2015
|
MTWARA
|
15
|
8
|
23
|
|
JUMLA
|
304
|
76
|
380
|
No comments:
Post a Comment