TANZANIA OLYMPIC
COMMITTEE (TOC)
KAMATI YA OLIMPIKI TANZANIA
RISALA YA KATIBU MKUU (TOC), FILBERT BAYI KWENYE
UFUNGUZI WA KAMISHENI YA WANAMICHEZO ZANZIBAR TAREHE 10/12/2015.
Ndugu Mgeni Rasmi Jamal Adi, Katibu Mkuu
Msaidizi TOC
Ndugu Gulam Rashid, Rais wa TOC,
Ndugu Ramadhani Zimbwe, Mwenyekiti,
KAWATA Taifa,
Ndugu Amina Ahmed, Katibu KAWATA Taifa
Viongozi Kamati yaUtendaji Waalikwa
Kamati ya Utendaji, KAWATA Taifa,
Wanamichezo Washiriki
Mabibi na Mabwana.
Kwa
niaba ya Kamati ya Olimpiki Tanzania na kwa niaba yangu mwenyewe sina budi kumshukuru
Katibu Mkuu Msaidizi wa TOC, pamoja na kuwa moja wa viongozi wa juu wa TOC kukubali
mwaliko wa ofisi ya TOC kwa kuja hapa leo kutufungulia Mkutano huu Mkuu wa Kamisheni ya
Wanamichezo.
Ndugu
Mgeni Rasmi, ofisi ya TOC imekuwa hapo awali ikialika wageni rasmi hasa katika
shughuli hizi za ufunguzi wa mikutano yetu kutoka nje hasa taasisi na serikali,
lakini kuanzia sasa itakapobidi shughuli hizi zitafanywa na viongozi wa TOC au
Vyama/Mashirikisho ya Michezo.
Ndugu
Mgeni Rasmi, tangu Kamisheni ya Taifa ilipoundwa hapo mwaka 2006, kazi kubwa
ilikuwa kuhamasisha na kutoa wito kwa Vyama/Mashirikisho ya Michezo kuanzisha
Kamisheni ya wachezaji katika Vyama/Mashirikisho yao ya Michezo. Ni Vyama/Mashirikisho
chache ambayo yameitikia wito wetu kwa kufanya uchaguzi halali wa kidemokrasia.
Vyama
vingi mpaka sasa vimekuwa vikiteua wajumbe wake kuhudhuria Mikutano Mikuu ya Kamisheni
inayoandaliwa na TOC, lakini cha kushangaza kwa utafiti ulioofanywa na
TOC/KAWATA Taifa, wachezaji hao siyo wajumbe katika Kamati za Utendaji na
Mikutano Mikuu ya Vyama na Mashirikisho husika kama Muongozo wa Kamisheni
unavyosema.
Sijui
ni kwa nini Vyama/Mashirikisho ya Michezo yaogope kuwaingiza wachezaji kwenye
chombo cha maamuzi (Kamati ya Utendaji/Mkutano Mkuu). Kuna siri gani kubwa
katika vikao vya Kamati ya Utendaji na Mkutano Mkuu ambayo hayapaswi wachezaji
kufahamu?
Mimi
nina imani kabisa wawakilishi wa wachezaji watakapokuwa kwenye vyombo hivyo vya
maamuzi malalamiko na manung’uniko mengi ya wachezaji hayatakwepo, kwani
watakuwa wameshiriki kikamilifu katika maamuzi.
Mahali ambako Mkutano Mkuu wa Kamisheni ya Wachezaji (Kawata) unapofanyikia leo Zanzibar. |
1. Kutoa ushauri, nasaha kwa wanamichezo waliostaafu na
ambao bado wanaendelea na michezo.
2. Kulinda maslahi ya wanamichezo ndani ya maadili ya
Olimpiki.
3. Kutoa mapendekezo kwa mambo yanayohusu maslahi ya
wanamichezo ndani ya vikao ya Kamisheni husika.
4. Kufanya lolote lile ambalo ni kwa faida ya wanamichezo
kwa ujumla wake.
Kamisheni
yetu ya Kitaifa tangu ianzishwe mwaka 2006 na wajumbe wake Kitaifa kuchaguliwa
tena mwaka 2012 mjini Dodoma imechelewa
kwa kiasi fulani kutokana na sababu ambazo ni pamoja na kukwamishwa na viongozi
wa Vyama/Mashirikisho yao Kitaifa (NFs).
Baadhi ya washiriki wa Mkutano Mkuu wa Kawaita mjini Zanzibar leo Alhamisi. |
Mhe.
Mgeni Rasmi, michezo kwa sasa ni ajira, ndiyo maana IOC imehamasisha NOCs
kuunda Kamisheni za Wanamichezo ili watambuliwe kuwa sekta muhimu ya maendeleo
ya michezo katika Taifa letu.
TOC inaamini kwamba kukiwa na uwakilishi wa
wanamichezo katika vyama/mashirikisho ya michezo na asasi za umma nchi yetu
itakuwa imepiga hatua katika kupiga vita madawa ya kuongeza nguvu katika
michezo ambayo kwa sasa yamepamba moto duniani.
Baadhi ya waalikwa katika mkutano Mkuu wa Kamisheni ya Wachezaji Tanzania (Kawata) Kutoka kushoto Irine Mwasanga, Peter Mwita na Mwinga Mwanjala wakati wa mkutano huo leo Zanzibar. |
Kwa
haya machache naomba nikukaribishe ili uzungumze na wanamichezo walio mbele
yako kisha utufungulie Mkutano huu wa Kamisheni ya wanamichezo kwa mwaka 2015
kama tulivyokuomba.
Ahsanteni kwa kunisikiliza.
Katibu Mkuu wa TOC Filbert Bayi akifuatilia jambo na mjumbe wa Kamati ya TOC Irine Mashanga wakati wa Mkutani Mkuu wa Kawata Zanzibar leo. |
No comments:
Post a Comment