Olivier Giroud alikuwa shujaa wa Arsenal wakati alipofunga hat-trick na kuiwezesha Arsenal kuifuna Olympiacos na kutinga hatua ya mtoano ya 16 bora |
ANTHENS, Ugiriki
LIVIER Giroud alifunga mabao matatu mwenyewe (hat-trick) wakati Arsenal
ikijihakikishia nafasi ya kufuzu kwa hatua ya
16 bora ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya kwa kuifunga Olympiakos mabao 3-0.
Ikihitaji ushindi wa mabao angalau mawili kwa bila ili ifuzu kwa
hatua hiyo, the Gunners ilionesha kiwango kizuri na kujikuta ikimaliza ya pili
katika Kundi F.
Giroud alifunga la kwanza katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo
kabla hajafunga tena katika kipindi cha pili baada ya kazi nzuri iliyofanywa na
Joel Campbell.
ARSENAL
YAENDELEZA REKODI
Arsenal haijawahi kushindwa kutinga hatua ya mtoano ya Ligi ya
Mabingwa wa Ulaya tangu michuano hiyo ilipoanza mfumo mpya katika msimu wa
mwaka 2003-04, na uzoefu wao ulidhihirika usiku wa jana katika mchezo huo uliofanyika
jijini hapa.
Arsenal iliuanza mchezo huo kwa kasi huku wenyeji wakicheza na
kuungwa mkono na mashabiki wa nyumbani waliokuwa wakishangilia bila kuchoka.
Mathieu Flamini alikaribia kufunga baada ya mpira alioupiga
kugonga mwamba kabla Giroud hajafunga la kwanza kwa kichwa cha karibu na lango
akiunganisha krosi ya Aaron Ramsey.
Giroud akifunga kwa kichwa katika dakika ya 29 dhidi ya Olympiacos katika mchezo dhidi ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya katika mchezo wa Kundi F |
Bao la pili lilikuwa bora kwa usiku huo wakati Giroud alilifunga
baada ya kukimbia na mpira kutoka katika mstari wa nusu ya uwanja kabla
hajapiga na kuujaza mpira wavuni.
Bao la tatu ni la penalty, ambapo Omar Elabdellaoui aliunawa mpira
uliopigwa na Nacho Monreal na Giroud alifunga kirahisi.
NINI KINACHOFUATA?
Arsenal ilifanya vizuri na kufuzu baada ya kufungwa mechi za awali
mbili dhidi ya Dinamo Zagreb (2-1 ugenini) na Olympiakos (3-2 nyumbani) ikiwa na maana kuwa ilishindwa
kabisa kupata hata pointi moja katika kundi lao baada ya kucheza mechi mbili.
Timu hiyo iliendelea kupata kisago kwa kufungwa 5-1 na mshindi wa
kundi hilo, Bayern Munich katika mchezo uliofanyika Ujerumani baada ya kushinda
2-0 dhidi ya kikosi cha kocha Pep Guardiola katika mchezo uliofanyika England.
Sasa wamemaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Bayern ikiwa na
maana kuwa timu hiyo sasa itakutana na ratiba ngumu wakati wa upangaji wa
ratiba hiyo ya 16 bora ukilinganisha na timu hiyo ya Ujerumani.
Timu inazoweza kukutana nazo ni pamoja na vigogo ya Hispania Real
Madrid, Atletico Madrid na Barcelona, Wolfsburg kutoka Ujerumani au ile ya
Russia ya Zenit St Petersburg.
Wataungana na ndugu zao wa Chelsea na Manchester City katika
ratiba hiyo itakayopangwa Jumatatu
UNACHOTAKIWA
KUJUA
Olivier Giroud ni mchezaji wanne wa Arsenal aliyewahi kufunga hat-trick
katika michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya (baada ya Thierry Henry, Nicklas
Bendtner na Danny Welbeck).
Hii ni mechi ya kwanza kwa kikosi cha Arsene Wenger kushinda
nchini Ugiriki tangu Desemba mwaka 1998 (wakati walipoifunga Panathinaikos kwa
mabao 3-1).
Matokeo hayo yanamaliza umwamba wa kutofungwa kwa timu hiyo ya Ugiriki
dhidi ya zile za Uingereza
No comments:
Post a Comment