Na Mwandishi Wetu
SHULE ya msingi ya Hazina imeshika nafasi ya kwanza katika mkoa wa
Dar es Salaam katika mtihani wa utamilifu wa darasa la saba uliofanyika Juni 4 na
5 mwaka huu.
Ofisa Elimu mkoa wa Dar es Salaam Raymond Komba aliipongeza shule
hiyo, ambayo pia ilitoa mwanafunzi wa kwanza hadi wa 10 katika mtihani hiyo.
Majengo ya shule ya Msingi Hazina yaliyopo Magomeni jijini Dar es Salaam, ambako wanafunzi walioshika nafasi 10 katika mtihani wa Utamilifu na kuzipita shule zote za mkoa huo. |
Komba aliyasema hayo katika kikao cha watendaji wa elimu mkoa wa
Dar es Salaam, walimu wakuu, wazazi na baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri
katika mtihani huo wa majaribio.
Aliipongeza shule ya Hazina kwa kushika nafasi ya kwanza kimkoa katika
matokeo yote yaliyojumuisha shule za binafsi pamoja na zile za serikali, huku
wanafunzi wake wakishika nafasi ya kwanza hadi ya 10.
Usafiri sio tatizo katika shule ya Hazina, Hilo ni moja ya mabasi ya shule hiyo ambayo hufanya wanafunzi kutohangaika katika usafiri. |
Wanafunzi wa shule hiyo walioshika nafasi ya kwanza hadi ya 10 ni Rajabu
Said, Atif Mustifa, Zauditu Ally, Baraka Juma, Tatiana Ally, Warda Agapiti,
Witness Jonas Mallosa, Henry Flowin Madiwa, Henry Godfrey Msuya na Ismail
Khaliphan.
Jumla ya wanafunzi 58,489 kati ya 59,709 waliosajiliwa walifanya
mtihani huo kwa mkoa wa Dar es Salaam, huku shule ya Kijitonyama Kisiwani
ikiibuka ya kwanza kwa upande wa shule za serikali pekee.
Mapunda alisema kuwa ufaulu wa kila shule ndio unaotafsiri ufaulu
wa wilaya na kuamua ufaulu wa Manispaa kwa ujumla, hivyo alizitaka shule
kungeza juhudi wakati wa kuelekea katika mtihani wa taifa wa darasa la saba
utakaofanyika Septemba 9-10.
Pia, ofisa huyo elimu alizipogeza shule za mkoa wa Dar es Salaam
kwa kushika nafasi ya kwanza katika mtihani wa taifa mwaka jana na kuwataka
kufanya vizuri zaidi mwaka huu ili kuendelea kuishikilia nafasi hiyo.
Akizungumza na gazeti hili mwanafunzi aliyeshika nafasi ya kwanza
Rajabu Said alisema kuwa wamefanya vizuri kutokana na jitihada za bila kuchoka
za walimu wao pamoja na wao kuwa wasikivu na kuelewa kile wanachofundishwa.
Pia, aliahidi shule yao kuendelea kuibuka ya kwanza katika mtihani
wa kitaifa utakaofanyika mwezi ujao.
Mwanafunzi aliyefanya vizuri zaidi katika mtihani huo kwa kushika nafasi ya kwanza, Rajabu Said akihojiwa baada ya kutangazwa mshindi. |
Rajabu Said akipongezwa na Ofisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Komba. |
No comments:
Post a Comment