KUNDI mahiri la muziki nchini Kenya la Sauti Sol jana liliwasili
nchini tayari kwa onesho kabambe la muziki la Party in the Park litakalofanyika
kwenye viwanja vya Farasi nyuma ya shule ya Oyesterbay jijini Dar es Salaam.
Kundi hilo lilitua kwenye Uwanja wa Mwalimu Nyerere saa 3:15 kwa
ndege ya Kenya Airways na baadae kuimba kibao cha `Sura Yako Nzuri’ mara walipotoka nje ya uwanja ambako walikutana na waandishi wa
habari.
Akzungumza na waandishi wa habari wanamuziki hao walisema kuwa,
wamekuja kutoa shoo ya kufa mtu, ambapo waliwataka Watanzania kujitokeza kwa
wingi kuwashuhudia.
Msanii mmoja wa kundi hilo Savara Mudigu alisema kuwa wamejipanga
vizuri na kuwataka wapenzi wa muziki kufika kushuhudi makali yao kikiwemo kibao
chao cha `Sauti Yako Nzuri’ ambacho
kinapigwa sana na vituo mbalimbali vya radio na Tv hapa nchini.
Mwanamuzikimwingine wa kundi hilo, Polycarp Otieno alisema kuwa
hii itakuwa mara yao ya nne kupiga muziki nchini Tanzania na ni mara yao ya
tatu kupiga jijini Dar es Salaam na mara moja waliwahi kupiga Mwanza.
Aliwataka wapenzi wa muziki kukaa mkao wa kula kwani wamejipanga
vizuri kung’ara katika tamasha hilo
litakaloshirikisha pia makundi ya Afrika Kusini na Tanzania.
Wanamuziki wa Tanzania watakaofanya vitu katika tamasha hilo ni
Ali Kiba pamoja na Feza Kessy wakati makundi ya Afrika Kusini ni pamoja na
Mafikizolo, Beatenberg na Black Motion.
No comments:
Post a Comment