Na Waandishi Wetu
DK. John Pombe Magufuli (pichani), mgombea wa Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), amezindua kampeni zake za
kuwania nafasi hiyo ya uongozi katika viwanja vya Jangwani jijiniDar es Salaam.
Maguuli aliuambia umati mkubwa wa watu uliojitokeza kumsikiliza, ambapo alisema kuwa ameomba kibarua hicho cha kuiongoza Tanzania kwa ajili ya kuleta mabadiliko ya kweli kwa umma.
Kwa hali hiyo amewaomba
Watanzania waichague CCM na waache jazba ya kukiua chama hicho kwani yeye
pamoja na mgombea wake mwenza wamedhamiria kuleta mabadiliko ya kweli kwani
wanatambua kuwa wananchi wanataka mabadiliko yenye kuwaleta maisha mazuri.
"Natambua kuwa Watanzania mnataka maisha mazuri, naahidi
kukomesha wizi na rushwa haraka kwa sababu palipo na rushwa hakuna maendeleo,"
alisema Dk John Magufuli.
Aliahidi kushughulikia kero za wakulima ambao alisema wanataka
wapate pembejeo na mbegu bora kwa bei nzuri pamoja na uhakika wa soko la mazao
yao. Alisema akichaguliwa itakuwa mwisho wa mkulima kuikopesha Serikali.
Mgombea huyo alihoji inakuwaje mkulima anaikopeshe serikali badala ya Serikali
kumkopesha mkulima.
Aliahidi kujenga umoja wa kitaifa kwani taifa mabalo halina umoja
haliwezi kujiletea maendeleo, kwa hali hiyo akasema ataendelea kupiga vita
ukabila, ukanda na udini kwani ndio utanzania mbao amepanga kuujenga akiwa
Rais.
Aliahidi kulinda muungano na kurekebisha dosari ndogondogo, lakini
zaidi alisema serikali yake itaendeshwa kwa kuheshimu mipaka ya mihimili ya
dola. Alisema angependa awe na Bunge ambalo litaisimamia vizuri Serikali na
akatoa mwito kwa wananchi kuchagua Wabunge wengi wa CCM ili wawe wakali kwa
serikali yake.
Aliahidi kuunda mahakama itakayoshughulikia kesi za rushwa na
ufisadi. "Nitabanana nao polepole ili wananchi waweze kupata haki zao
kwani vitendo vya ufisadi ndivyo vilivyoifikisha hapa nchi ilipo.
Mgombea huyo wa CCM aliahidi kuheshimu utawala bora, pia alisema
serikali yake itaheshimu mawazo mazuri
yatakayotolewa na vyama vingine vya siasa ambayo mwelekeo wake ni kulijenga
taifa.
"Nasema hivyo maana mimi naamini kwamba maendeleo hayana
vyama, ninachotaka mimi ni kazi tu ili maendeleo yaweza kusonga mbele,"
alisema.
Pia aliahidi kuimarisha vyombo vya ulinzi na usalama hasa jeshi la
polisi kwa kulipatia vifaa vya kisasa. Alisema ni aibu kwa askari polisi
kuvamiwa na majambazi akapigwa hadi akanyang'anywa silaha hivyo akasema
serikali yake itataka kuona askari hao wanakuwa na vifaa vya kisasa lakini pia
wanaishi kwenye nyumba bora zaidi.
AJIRA:
Kuhusu ajira Dk Magufuli
alisema serikali yake itaongeza ajira kwa vijana ana akasema njia pekee ya
kufikia malengo hayo ni kujenga viwanda vingi ambavyo vitasaidia kulimaliza
tatizo hilo. Alisema miongoni mwa viwanda atakavyojenga kwa kushirikiana na
sekta binafsi ni viwanda vya kuchakata samaki.
"Samaki ambao kwa sasa tunaibiwa huko baharini na wanapelekwa
nje, sasa watatengenezewa hapa hapa na hilo linawezekana maana tutalifanya kwa
kuleta wawekezaji kutoka nje bila kuwepo urasimu. Maafisa serikalini ambao
wamezoea urasimu wa njoo kesho ambayo inakwamisha uwekezaji, nawaambia watafute
sehemu nyingine ya kuishi."
Katika eneo hilo la viwanda, Dk Magufuli alisisitiza kuwa hakuna
haja ya kuuza marobota ya pamba nje ya nchi; badala yake dawa ni kujenga
viwanda vya kutengeneza khanga na vitenge. "Badala ya kuuza nanasi zima
kutoka Msoga kwa mheshimiwa Rais Kikwete (Jakaya) sasa tutauza juisi hapa hapa
nchini."
Alisema iwapo Serikali itajenga viwanda vingi, ajira itaongezeka
kwa asilimia 40. Alisema viwanda vingine ambavyo vitajengwa viwanda vya nyama
na maziwa kwa ajili ya kuwasaidia wafugaji ambao kwa sasa wahamahama na mifugo
yao.
"Haya ndio maendeleo ninayoyataka," alisema Dk Magufuli
ambaye alitumia saa moja jana kujinadi wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama
hicho ambao ulihudhuriwa na maelfu ya watu katika viwanja vya Jangwani, Dar es
Salaam.
Alisema licha ya juhudi zinazofanywa na Serikali za kuwasaidia
wachimbaji wadogo, lakini yeye akiingia madarakani anatahakikisha kundi hilo
linaboreshewa mahitaji yake zaidi ili waweze kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi.
Pia aliahidi kupunguza tatizo la utoroshaji wa madini nje ya nchi
na akaoa mfano kuwa inakuwaje Tanzania ambayo inachimbwa Tanzania pekee leo hii
nchi ya kwanza kuuza madini hayo ni India na kufuatiwa na Kenya na Tanzania
inashika nafasi ya tatu "Hili nitaliangalia kwa kina."
MAJI, AFYA NA ELIMU:
Alisema Serikal iyake itahakikisha asilimia 87 ya Watanzania
walioko vijijini wanapata maji safi na salama na asilimia 95 ya wakazi wa
mijini watapata huduma hiyo. Alisema ili kupunguza kero kwa akina mama,
watajitahidi huduma hiyo inapatikana karibu na yalipo makazi ya watu.
Alisema pia watajenga zahanati kila kijiji na vituo vya afya kila
kata ili kuhakikisha kuwa watanzania wanapata huduma za afya kwa ufanisi.
Kwa upande wa elimu, alisema watahakikisha wanafunzi wanasoma bure
kuanzia shule ya msingi hadi kidato na nne. Alisema fedha za kutekeleza mpango
huo zitapatikana tu pale atakapobana mianya ya rushwa na ufisaidi serikalini.
Pia aliahidi kujenga nyumba za walimu kwa wingi ili waweze kupata
sehemu nzuri ya kukaa pamoja na kuendeleza juhudi za kujenga mabweni katika
shule mbalimbali ili kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu katika mazingira
mazuri.
Kwa pande wa wanafunzi
wanaosoma vyuo vya elimu ya juu, alisema atakachofanya ni kuhakikisha kuwa
wanapatiwa mikopo yao kwa wakati na sio kucheleweshewa.
"Inakuwaje mkopo unacheleweshewa mtu wakati ni mkopo,
inakuwaje mwanachuo kupatiwa mkopo hadi agome kwanza? Alihoji mgombea huyo na
kusema kuwa atahakikisha mwanafunzi akienda chuo anapatiwa mkopo wake kwa
wakati na kazi yake itakuwa ni kusoma peke yake na sio kufuatilia masuala ya
fedha.
MIUNDOMBINU:
Dk Magufuli alisema kazi ya kwanza atakayoifanya ni kuhakikisha
wanaunganisha makao makuu ya mikoa yawe na barabara ya lami na baadaye wataenda
kuunganisha na wilaya zote.
Alisema pia watajenga barabara ya kisasa ya njia sita kutoka Dar
es Salaam hadi Chalinze ambayo itakuwa
na barabara za ghorofa zipatazo saba. Alisema pia kuwa ujenzi wa barabara ya
ghorofa katika makutano ya Tazara karibu utaanza kwani kampuni ya kijapani
tayari imeshaanza kufanya kazi hiyo
Alisema atajenga reli na kuboresha bandari ili kuhakikisha uchumi
wa nchi unaimarika zaidi kwani anaamini kuwa miundombinu hiyo ndio njia pekee
ya kuboresha uchumi wa nchi. Alisema katika kukamilisha mambo hayo, serikali
yake itakuwa rafiki wa wawekezaji na wafanyabiashara.
Maslahi ya wafanyakazi, vyombo vya habari, wasanii
Maslahi ya Wafanyakazi, Dk Magufuli alisema atapenda kuona walimu
wanakuwa na maslahi mazuri pamoja na wafanyakazi wengine. Alisema ataboreha
maslahi yao ili wasiwe wanaingia ofisini saa nne na kutoka saa tano asubuhi.
Alisema ataboresha maslahi ya kada hiyo ili wafanye kazi kuanzia
asubuhi hadi jioni na watoke na mishahara mizuri.
Pia aliahidi kulienda uhuru wa habari ili waandishi wa habari
waendelee kufanya kazi zao katika mazingira mazuri. Alisema angependa kuona
waandishi wa habari wanakuwa na chombo chao za kutetea maslahi yao ili
atakapochaguliwa tu ahakikishe anakutana na chombo hicho kuangalia namna ya
kuboresha maslahi ya wanahabari.
Aliahidi pia kuanzisha mfuko wa wasanii pamoja na wanamichezo ili
waweze kunufaika na kazi zao "Nawaahidi kuwa sitawatumia kwenye siasa tu
bali pia nitaangalia maslahi yenu."
hodi ni wewe katika haraka haja mkopo kulipia kuanza yako madeni ya kuanzisha biashara au nyumba ??? Kisha inakuja teksi kampuni una imani na relay juu ya 100% uhakika sababu hii ni kampuni ambapo i cashed mkopo wangu kwa mama yangu Stella dawa leo ili kuwasiliana na René Mikopo Firm halisi kupimwa na kuaminiwa na leo mimi nina furaha i got mkopo wangu wa $ 120,000 leo ili kupata kushikamana leo mrsstellareneloanfirm@hotmail.com} {barua pepe hapa chini na kupata jibu la matatizo yako yote kwa sababu Siwezi Kunyamaza ushuhuda huu mkubwa peke yangu binafsi ili i aliamua kuandika kwenye tovuti kwa sababu kula furaha kubwa kwa yangu moyo na leo mimi nina kuishi maisha mapya shukrani kwa wote Stella René
ReplyDeletekolochatechee