Katibu
Mkuu, Kamati ya Olimpiki Tanzania Ndugu
Filbert Bayi
Viongozi wa Vyama vya Michezo
(TAHA/ZAHA)
Mkufunzi wa Kimataifa,
Waratibu wa Mafunzo (TOC na TAHA/ZAHA)
Washiriki wa Mafunzo,
Mabibi na Mabwana.
Napenda
kuchukua nafasi hii kuishukuru TOC na TAHA/ZAHA kwa kunipa heshima hii ya kuwa
mgeni rasmi katika kufunga mafunzo haya ya walimu wa mchezo wa Mpira wa Mikono.
Ni
matumaini yangu kuwa mmepata dozi nzuri ya taaluma na mbinu mbalimbali ya
kufundisha mchezo huu. TOC inauthamini sana mchezo wa mpira wa mikono, kwani ni kati ya michezo
ambayo TOC inaamini kuwa ni baadhi ya michezo iliyokuwa inapendwa sana na
watanzania pamoja na kuchezwa katika Mikoa michache hasa na vilabu vya Majeshi
yetu (Polisi, JWTZ, Magereza, JKT/JKU nk.
Kama
kweli tunataka mchezo huu uenee nchi nzima, vyama husika havina budi kufanya
jitihada ya kufufua vyama vya mchezo huu Mikoani kama vipo na kuanzisha
katika Mikoa ambayo havina vyama hivyo,
hali kadhalika na kuueneza katika Shule zetu za Msingi na Sekondari ambapo
ndipo penye vipaji vingi. Tusisubiri tu wakati wa Michezo ya Umisseta na
Umitashumta Taifa.
Kama
nilivyofahamishwa vyema haya ni mafunzo ya pili
kufanyika kwa walimu wetu hapa Tanzania. Mafunzo ya awali kwa walimu yalifanyika
mjini Dar Es Salaam mwaka 2007 yote
yakifadhiliwa na Olimpiki Solidariti
kupitia Kamati ya Olimpiki Tanzania.
Pia
naamini mmefaidika na elimu mliopata kutoka kwa mtaalamu wa Kimataifa Ndugu
Tuma ambaye amekuwa wakiwaandalia masomo yote ya nadharia na vitendo kwa muda wote
wa siku 11. Ni mategemeo yangu elimu mliyopata itawasaidia kuandaa timu zenu na
kutambua vipaji vipya katika maeneo mnayotoka. Ni ukweli usiopingika
kwamba mmejiongezea elimu ya kufundisha
mchezo huu wa mpira wa mikono kwa kiwango cha hali ya juu, mkilinganisha uwezo na
elimu mliyokuwa nayo awali na wachezaji wa taifa kufaidika kwa ushiriki wao wa
mara ya kwanza.
Wakati
wote nimewahi kusikia TOC kuwa mstari wa mbele katika kuendeleza taaluma ya
ufundishaji na mbinu za kisasa za kuboresha uwezo wa walimu, ili waweze kufikia
viwango vinavyotakiwa kwa timu zetu zinaposhindana katika mashindano mbalimbali
ya Kimataifa.
Ningependa
kusisitizia sana kwenu walimu mnaomaliza mafunzo haya kwamba, mhakikishe mchezo
huu wa mipra wa mikono unapiga hatua
kufikia kiwango ambacho kitatupeleka kwenye michezo ya Kanda, Afrika na
Kimataifa.
Tanzania
haina tofauti na nchi kama Misri, Algeria, Nigeria, Tunisia nk ambao zimekuwa tishio katika mchezo wa mpira
wa mikono katika bara letu la Afrika.
Ningependa
kuwasihi walimu mnaomaliza mafunzo haya leo kuupeleka mchezo huu mashuleni
walipo vijana wengi wenye vipaji vingi ambao wanafundishika na rahisi kuelewa.
Inahitajika mipango mahususi ya mazoezi na mashindano ambayo nina imani Vyama
vyetu vya Mpira wa Mikono Tanzania Bara na Zanzibar wanayo mipango hiyo.
Wizara
zinazoshughulikia michezo Tanzania zimetayarisha mipango kwa kushirikiana na
vyama vya michezo kuendeleza michezo ya aina yote. Linalotakiwa hivi sasa ni
kwa walimu wetu kutumia mafunzo haya katika kuendeleza mchezo wa mpira wa mikono
nchini. Changamoto itoke kwenu ili Vyama, Mabaraza na Wizara husika na wanamichezo
baadhi yao ambao wako hapa leo waweze kuchangamkia mipango yenu mtakayoandaa.
Napenda
nichukue nafasi hii kumpongeza na kumshukuru mtaalamu wa Kimatafa Ndugu Tuma
kwa jitihada zake za kutoa mafunzo haya kwa ufanisi mkubwa, waratibu wa TAHA/ZAHA,
TOC na Walimu washiriki kwani bila wao kuwepo hapa mafunzo haya yasingefanyika.
Nitakuwa
mchoyo wa fadhila kama sitawashukuru Olimpiki Solidariti kwa kufadhili mafunzo
haya, Shirikisho la Kimataifa la mpira wa mikono (IHF) kwa kumteua Mkufunzi niliyemtaja hapo juu kuendesha
mafunzo, TOC na TAHA/ZAHA kwa maandalizi mazuri, mwisho kabisa nawashukuru wale
wote waliohusika katika kufanikisha mafunzo haya kwa namna moja au nyingine
hasa waratibu wa TOC na TAHA/ZAHA, Taasisi ya Filbert Bayi kama mwenyeji kwa
huduma zote nzuri mpaka kufika siku hii
ya mwisho.
Kwa
haya machache sasa natamka kwamba mafunzo yenu ya ualimu wa mchezo wa Mpira wa Mikono ninayafunga rasmi.
Ahsanteni!
No comments:
Post a Comment