Serena Williams akiwa na taji lake la Cincinnati Masters |
OHIO, Marekani
SERENA Williams na Roger Federer mwishoni mwa wiki walitwaa
ubingwa wa tenisi wa mashindano ya Cincinnati Masters kwa upande wa wanawake na
wanaume.
Williams ambaye ni bingwa namba moja kwa ubora duniani kwa upande
wa wachezaji tenisi wanawake, alimshinda bingwa namba tatu Simona Halep na
kutwaa taji hilo.
Mchezji huyo mwenye umri wa miaka 33 alishinda mchezo huo kwa 6-3
7-6 (7-5) na kumsambaratisha Mromania Halep, mwenye umri wa miaka 23,ambaye kwa
kucheza fainali ya mashindano hayo tayari alishapangwa katikanafasi ya pili ya
kushiriki mashindano ya US Open.
Halep alimzidi Williams mwanzoni mwa mchezo, lakini bingwa huyo wa
Wimbledon alipambana na kushinda mchezo huo.
"Shukrani kwa Simona kwa kucheza mchezo mzuri kama ule, "
alisema Mmarekani huyo, ambaye alishinda mchezo huo kwa kutumia saa moja na
dakika tisa.
"Siungwi mkono kokote ninakocheza, lakini hapa nimeoneshwa
upendo mkubwa na ninataka kurudi tena.”
Halep alisema: "Ni furaha ilioje kwa yeye kucheza fainali.
Anampongeza bingwa.”
Naye Roger Federer alitwaa ubingwa huo baada ya kumshinda bingwa
namba moja kwa ubora Novak Djokovic na kushinda taji la saba la Cincinnati
Masters.
Mchezaji huyo Mswis mwenye umri wa miaka 34, aliyemtoa Muingereza Andy
Murray katika nusu fainali, alipata ushindi huo kwa 7-6 (7-1) 6-3.
Federer, ambaye sasa atapangwa katika Kundi la Pili katika
mashindano ya US Open, alishindamchezo huo kwa saa moja na dakika 30.
Roger Federer akipozi na kombe lake. |
No comments:
Post a Comment