Jukwaa jipya litakalotumika katika tamasha hilo likijengwa kwa ajili ya majaribio kabla ya kuhamishiwa kwenye viwanja vya Farasi nyuma ya shule za Oysterbay jijini Dar es Salaam. |
MAANDALIZI ya tamasha kubwa la muziki la Party in the Park
litakalofanyika Jumamosi na kuwashirikisha wasanii wa Tanzania, Kenya na Afrika
Kusini yamepamba moto huku tiketi zikinunuliwa kama njugu.
Tamasha hilo la aina yake litafanyika kwenye viwanja vya Farasi au
The Green nyuma ya shule ya msingi na sekondari ya Oysterbay katika barabara ya
Kenyatta.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mratibu wa tamasha hilo,
Harry Magere alisema kuwa tayari wameanza kufunga jukwaa na maandalizi mengine
ili kuhakikisha onesho hilo linafana.
Magere akizungumzia kiingilio alisema tayari tiketi za sh. Milioni
1.5 zimeshamalizika, ambapo meza moja itakuwa na viti sita na mteja wa meza
hiyo atakuwa na mahali maalum pakuegesha gari lake.
Mbali na nafasi ya kuegeshea gari moja, pia watakaokaa katika meza
hiyo watapewa chakula na vinywaji vya kuanzia.
Wanamuziki wa Tanzania, Alikiba na Feza Kessy walipozungumza na waandishi wa habari kuhusu tamasha hilo. |
Alisema kuwa maandalizi yote yanakwenda vizuri na wanamuziki wa Sauti
Sol kutoka Kenya watawasili Ijumaa asubuhi wakati wale wa makundi ya Afrika
Kusini wanatarajia kuwasili siku hiyo usiku tayari kwa shoo hiyo kabambe.
Wasanii wa Afrika Kusini waliomo katika ratiba hiyo ya kutumbuiza
katika tamasha hilo ni kutoka makundi ya Mafikizolo, Beatenberg na Black Motion
wakati baadhi ya wasanii wa Tanzania watakuokuwepo ni Alikiba, Feza Kessy na wengineo.
Aidha, Given Sandy akizungumzia kuhusu misosi siku hiyo alisema
wamejipanga vizuri na wapenzi wa muziki watarajie kupata pizza za uhakika zenye
viwango vya kimataifa.
Sandy ambaye ndiye meneja wa Eaters Point, ambazo ni mahiri kwa
misosi alisema kuwa, timu yake imejipanga vizuri kwa ajili ya kutoa huduma
katika tamasha hilo la kimataifa.
Wadhamini wa tamasha hilo ni pamoja na Peps, KCB Bank, Eaters Point, Wantanshi, East Africa TV na Radio, Savanna
Wadhamini wa tamasha hilo ni pamoja na Peps, KCB Bank, Eaters Point, Wantanshi, East Africa TV na Radio, Savanna
No comments:
Post a Comment