MAMLAKA YA VIWANJA VYA
NDEGE TANZANIA
TANGAZO LA KIFO
Hayati Mhandisi Lambert W.
Ndiwaita
Bodi ya Ushauri,
Menejimenti na Wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA)
wanasikitika kutangaza kifo cha Mwenyekiti wa Bodi ya TAA,
Inj. Lambert W. Ndiwaita
kilichoteka tarehe
20/08/2015 katika Hospitali
ya Nairobi, Kenya. Marehemu anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwake
mjini Bukoba tarehe 25/08/2015.
Mhandisi Lambert Ndiwaita
(64) ni mmoja wa wataalamu waliobobea
katika masuala ya usafiri wa anga kitaifa na kimataifa, katika kipindi cha uhai
wake ametoa mchango mkubwa katika
maendeleo ya sekta hiyo hapa nchini na nchi nyingine duniadi.
Alianza shughuli zinazohusiana na
usafiri wa anga mwaka 19971
alipoajiriwa na iliyokuwa Wizara
ya Ujenzi kama
Mhandisi Msaidizi na baadaye
alipanda hadi kufikia cheo cha Mhandisi Mkuu
(Chief Engineer) akishughulikia masuala ya baeabara na viwanja vya ndege. Mwaka 1993 alikwenda
kufanya kazi katika Idara ya Usafiri wa Anga nchini Botswana kwa mkataba wa
mwaka mmoja.
Mwaka 1994 aliajiriwa na
Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga
International Civil Aviation Organization (ICAO) kusimamia
masuala ya viwanja vya ndege
(Aerodrome & Ground Aids) kwa eneo
la Mshariki na kusini mwa Afrika, katika ofisi za ICAO zilizopo jijini Nairobi, Kenya.
Mhandisi Ndiwaita ni msomi aliyehitimu Shahada ya kwanza ya
Uhandisi (Bsc Civil Engineering) katika Chuo Kikuu cha Nairobi. Mwaka 1978
alihitimu masomo Shahada ya Uzamili (Msc
in Civil Engineering) katika Chuo kikuu cha Califonia, Berkley, nchini Marekani
akijitikita zaidi katika masuala uhandisi wa ujenzi wa viwanja vya ndege.
Marehemu Lambert Ndiwaita atakumbukwa na
wadau wa usafiri wa anga nchini na duniani kwa mchango
mkubwa katika maendeleo ya sekta
hiyo ambapo kwa hapa nchini akiwa Mwenyekiti wa Bodi ya TAA
amechangia kufanikisha ujenzi na
uboreshaji wa viwanja kadhaa vikiwemo Mwanza, Tabora, Kigoma,
Songwe,Mafia, Mpanda, Bukoba na Julius Nyerere
(JNIA).
Mungu ailaze roho marehemu
mahala pema peponi.
Imetolewa na Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu-TAA.
24th AUGUST, 2015
Agosti 12, 2015
No comments:
Post a Comment