*Ni tiketi 20, mabegi na suti za michezo kwa ajili ya mashindano ya Afrika
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Covenant. Sabetha Mwambenja (kushoto) akizungumza kabla ya kukabidhi tiketi za ndege kwa timu ya Taifa Queens. Kulia ni nahodha wa timu hiyo Sophia Komba. |
Mwenyekiti wa Chaneta Annie Kibira (kushoto) akizungumza wakati wa kukabidhiwa tiketi za ndege na Covenant Bank leo asubuhi. |
Ofisa Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Allen Alex akizungumza wakati wa hafla hiyo. |
Nahodha wa timu ya taifa ya netiboli, Taifa Queens, Sophia Komba. |
Mkurugenzi wa Coenant Bank (kushoto) akimkabidhi tiketi mmoja wa wachezaji wa Taifa Queens. |
Na Cosmas Mlekani
BENKI ya Covenant leo imetoa tiketi 20 za ndege, mabegi na suti za
michezo kwa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta) ili kuiwezesha timu ya Taifa
Queens kwenda Gaborone Botswana kushiriki mashindano ya Afrika.
Mashindano hayo yanaanza Jumamosi na Taifa Queens inaondoka Ijumaa
na wachezaji 17 na viongozi watatu tayari kwa mashindano hayo makubwa barani
Afrika.
Benki hiyo ya wanawake ya Tanzania imetoa jumla y ash. Milioni 40
kwa ajili ya tiketi na vifaa hiyo vingine ambavyo itatumika na timu hiyo ikiwa
nchini Botswana.
Akizungumza wakati wa kukabidhi tiketi hizo katika Makao Makuu ya
benki hiyo Kijitonyama jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo
Sabetha M.J Mwambenja alisema kuwa wameisaidia Taifa Queens ili kuwawezesha
kushiriki mashindano hayo.
Alisema timu hiyo inaundwa na wanawake hivyo ni moja ya jukumu lao
kuwawezesha wanawake kufikia malengo yao kwa njia tofauti.
Mwakilishi wa Wizara ya Kazi, Vijana Utamaduni na Michezo Allen B.
Alex liishukuru benki hiyo kwa kubeba `msalaba’ wa wizara hiyo ambayo ni jukumu lake kuvisaidia vyama vya
michezo.
“Naishukuru
benki ya Covenant kwa kuchukua msalaba wa serikali wa kuvisaidia vyama vya
michezo kuisaidia Chaneta kupeleka timu Namibia “alisema Alex.
Alizitaka tasisi zingine kuiga mfano wa Cevenant Bank wa kusaidia
jamii.
Mwenyekiti wa Chaneta Annie Kibira aliishukuru benki hiyo hasa
mkurugenzi wake (Mwambenja) kwa kukubali kuisaidia Chaneta licha ya kuombwa kwa
muda mfupi.
“Nawapongeza
Covenant na hasa dada yangu (Sabetha) kwa kukubali kutusaidia licha ya
kuwasilisha maombi siku chache zilizopita “alisema.
Naye nahodha wa timu hiyo Sophia Komba alisema kuwa, wamejiandaa
izuri kwa ajili ya mchezo huo na wanatarajia kufanya vizuri katika mashindano
hayo.
No comments:
Post a Comment