NEW YORK, Marekani
MAMLAKA ya New York yameanzisha
uchunguzi kuhusu madai kuwa mwalimu mkuu msaidizi wakike alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi
wakike.
Mkuu huyo msaidizi, Pelagia
Papoutsis,mwenye umri wa miaka 33, aliondolewa
mkukumku kutoka katika shule ya sekondari ya William Cullen Bryant kabla ya
kuanza kwa vipindi mapema mwezi huu.
Papoutsis,mwalimu wazamani
wa hisabati katika shule iliyopewa jina la utani la "Pelly," alipandishwa
cheo hadi mwalimu mkuu mnsaidizi mwaka jana. Inaelezwa kuwa mwalimu huyo
alikuwa karibu na mkuu wake Namita Dwarka, kwa mujibu wa taarifa.
Mwanafunzi huyo wazamani anasema
kuwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Papoutsis. Madai yaliyotolewa baada
ya mwanafunzi huyo kuzungumza katika facebook na mwalimu wa gym Peter
Maliarakis.
Maliarakis alichangia ujumbe
huo na gazeti la New York Post.
“Pelly aliuwa na
mahusiano mabaya na mwanafunzi, “aliandika
mwanafunzi ambaye jina lake halikujulikana. “Mimi
nilikuwa shahhidi wa kwanza kwa sababu mimi nlihusika.”
Mwanafunzi huyo pia katika ujumbe
wake kwa Maliarakis akisema kuwa mkuu wa shule alikuwa akijua tatizo hilo lakini
“hakulifanyia kzi” na hakufanya kitu chochote.
Maliarakis aliliambia gazeti
la The Post: “alisema
uhusiano wao ulitokea wa mwaka wa mwisho. Alikuwa na umri wa miaka 17, na aliendelea
hata baada ya kumaliza shule.”
Tangu umri wa miaka 17, uhusiano
wa kimapenzi na mwanafunzi mwenye umri huo halikuwa shitaka la jinai lakini mtu
anaweza kuachishwa kazi ya ualimu mkuu msaidizi.
Regina Romain, msemaji wa Richard
Condon, kamati maalum ya uchunguzi kwa shule za mjini, alithibitisha kuwa uchunguzi
unaendelea. Alisema kuwa taarifa ya uchunguzi huo itachapishwa katika tarehe za
usoni.
No comments:
Post a Comment