HARARE, Zimbabwe
RAIS wa Zimbabwe mwenye umri
wa miaka 91 Robert Mugabe alisoma hotuba tofauti na ile aliyotakiwa kuisoma wakati
akifungua bunge la nchi hiyo hivi karibuni, kosa ambalo liliwafanya wapinzani kuhoji
uwezo wa kiakili wa kiongozi huyo mkongwe barani Afrika.
Mugabe, ambaye ni mtawala pekee
aliyebaki kusini mwa Afrika ambaye alitawala nchi hiyo tangu ilipopata uhuru wake
mwaka 1980, alisoma hutuba ile ile aliyoitoa Agosti 25, akiiomba China kusaidia
kufufua uchumi wa Zimbabwe.
Mugabe alimaliza hotuba hiyo
bila hata ya kuingiliwa, ambapo msemaji wake aliwalaumu viongozi huku akiahidi kuwa
rais huyo angeisoma tena hotuba hiyo katika siku ijayo.
"Mvurugano huo ulitokea
katika ofisi ya sekretari. Hotuba hiyo aliyoisoma bungeni ilitakiwa kuwekwa kando,
“alisema msemaji huyo wa rais George
Charamba.
Lakini chama kikuu cha upinzani
cha Movement for Democratic Change (MDC), ambacho kinakosowa utawala wake wa muda
mrefu,alisema utata huo unasababisha kuhoji uwezo wake wa kuendelea kuongoza.
Wakati huohuo, siku moja baada
ya kusoma hutuba hiyo kimakosa wakati wa ufunguzi wa bunge, wapinzani wameibuka
na kulaumu hatua ya rais huyo kutorudi tena bungeni na kusoma hutuba sahihi.
Jumanne, Bwana Mugabe, 91, aliyewasili
bungeni akiwa na gari lake la kipindi cha ukoloni la Rolls-Royce, alionekana kabisa
kutokuwa na habari kuwa hutuba aliyoisoma kwa takribani dakika 20 ni ile aliyoisoma
bungeni hapo mapema wiki tatu zilizopita wakati akilihutubia taifa.
No comments:
Post a Comment