NEW YORK, Marekani
MCHEZAJI tenisi nguli Serena Williams juzi alishindwa kutimiza ndoto yake ya kufanya
vizuri zaidi katika mashindano makubwa ya tenisi baada ya kutolewa katika
michuano ya US Open.
Williams, mwenye umri wa miaka 33, alijikuta akitupwa nje ya
mashindano hayo na mchezaji asiye hata na viwango katika orodha ya wachezaji wa
tenisi duniani Roberta Vinci wa Italia kwa seti 2-6 6-4 6-4.
Kipigo hicho kimemfanya Williams kushindwa kutinga fainali ya
mashindano hayo itakayofanyika leo jijini hapa.
Roberta Vinci wa Italia ndiye aliyemfunga Serena Williams na kumtupa nje ya mashindano ya US Open kwa seti 2-6 6-4 6-4. |
"Haya ni matokeo ya kushangaza zaidi katika historia ya
mchezo wa tenisi duniani, kwa sababu aliyepewa nafasi kubwa ndiye
aliyeondolewa.”
Williams aliaunza mchezo huo wa Ijumaa wa nusu fainali akiwa
ameshinda mechi 33 mfululizo za mashindano makubwa ikirejea nyuma ile ya Wimbledon
2014.
Mchezaji huyo alikuwa na matarajio ya kufikia rekodi ya Steffi
Graf ya mwaka 1988 ya kutwaa mataji wanne makubwa katika mwaka mmoja, na aliuwa
akicheza na mchezaji aliyemfunga mara nne bila ya kuambulia seti.
Vinci, 32, yuko katika namda 43 katika orodha ya ubora wa
wachezaji na kwa mara ya kwanza alikuwa akicheza nusu fainali ya mashindano
makubwa.
"Roberta Vinci, ni mcheaji mdogo, akiwa na rekodi ya
kushindwa na sasa anaingia katika mashindano ya US Open," alingeza Austin.
"Nilishinda mashindano matatu makubwa mwaka huu, " alisema
Williams. "Ndio, kama ningeshinda
mataji manne mfululizo ingewa jambo la faraja zaidi.”
No comments:
Post a Comment