BRISBANE, Australia
MTU
mmoja ambaye aligoma kuacha kuvuta sigara katika ndege kutoka Sydney kwenda Sunshine
Coast alijikuta matatani na kupigwa faini ya dola za Marekani 850 ikiwa ni mara
10 ya gharama ya njia moja ya tiketi.
Polisi
walisema kuwa mfanyakazi wa ndege alimuomba mtu huyo mwenye umri wa miaka 37
kuacha kuvuta sigara wakati wa safari hiyo ya ndege ambayo ingechukua dakika 90
jana, lakini alipuuza na kuendelea kupuliza moshi hewani.
Wakati
ndege hiyo ilipotua katika uwanja wa ndege wa Sunshine Coast majira ya saa
12:30 jioni, polisi waliingia ndani ya ndege hiyo na kumkamata mtu huyo.
Mtu
huyo kutoka Caboolture (Kaskazini ya Brisbane, Australia),kilometa 55 kusini
mwa pwani ya Sunshine na kufunguliwa mashtaka na anatakiwa kufika mahakamani
Oktoba 12, polisi ilisema.
Mapema
mwaka huu, abiria aliyepanda ndege hiyo ya Jetstar kutoka Gold Coast kwenda Sydney
aliwasha sigara katika chumba cha kupumzikia, na kulazimisha ndege kubadili
mwelekeo na kwenda Newcastle ambako ilitua kwa dharura.
Kuvuta
sigara kumepigwa marufuku ndani ya ndege za Australia na atakayepuuza amri hiyo
anapigwa faini ya dola za Marekani850.
No comments:
Post a Comment