Na Mwandishi Wetu
RIADHA Tanzania (RT), wiki hii ilipokea jozi za viatu 450 zenye
thamani ya sh. 45,000,000 kutoka kwa wananchi wa Finland.
Viatu hivyo vitasaidia katika maandalizi ya
wanariadha wa Tanzania kushiriki mashindano mbalimbali yatakayofanyika nje ya
nchi.
Akikabidhi viatu hivyo, Ari Koivu ambaye ni
Mkurugenzi Mtendaji wa wa taasisi ya Toiminnanjohtaja alisema kuwa, viatu hivyo
pamoja na samani za ofisi vimetolewa na watu wa Finland ili kusaidia maendeleo
ya michezo hapa nchini.
Alisema kuwa ameamua kutafuta vifaa hivyo kwa RT
kutokana na mapenzi yake kwa Tanzania ili kuendeleza michezo na hasa riadha
nchini.
Mbali na RT pia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Kitivo cha Sayansi ya Michezo, baadhi ya shule za msingi na sekondari za Mtwara na Lindi nazo zimefaidikana msaada kutoka Finland, ambao ni tofauti na ule waliopewa RT.
Alisema kuwa mpango wa maendeleo ya michezo mikoa hiyo ya kusini utafaidika na msaada huo.
Kaimu Katibu Mkuu wa RT, Ombeni Zavalla alisema
kuwa msaada huo umekuja wakati muafaka kwani sasa wanajiandaa kuanza mazoezi
kwa ajili ya mashindano mbalimbali ikiwemo Michezo ya Olimpiki itakayofanyika
Rio, Brazil mwakani.
Alisema kuwa viatu hivyo vitawasaidia sana
wanariadha kujiandaa vizuri kwa ajili ya mashindano mbalimbali, ambapo
aliwataka wadau wengi kujitokeza kusaidia mchezo huo.
Ari Koivu (kulia) akimkabidhi jozi ya viatu mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Riadha Tanzania (RT), Rehema Killo `Mbeya wa Mtaa'. |
Zacahria Gwandu, mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya RT akipokea jozi yake. |
Add caption |
Waandishi wa habari nao walipata mgao wa viatu na wengine jezi hivyo kutoka Finland. |
Dk. Hamad Ndee (katikati) wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam baada ya kukabidhiwa mgao wa chuo hicho. |
Add caption |
No comments:
Post a Comment