RIYADH, Saudi Arabia
SERIKALI ya Saudi Arabia imeanzisha uchunguzi ili kujua sababu za winchi
(Crane)kuanguka katika mji mtakatifu wa Macca, na kuuwa watu 107.
Winchi kubwa lenye rangi nyekundu liliangukia sehemu ya msikitiki
mkubwa uliokuwa umejaa waumini wakiendelea na ibada.
Taarifa zilisema kuwa upepo mkali na mvua kubwa ndio
zilizosababisha winchi hiyo kuanguka.
Ilielezwa kuwa awali kulikuwa na taarifa kuhusu rekodi ya usalama
katika eneo hilo la ujenzi la Saudi.
Msikiti huo mkubwa unaojulikana kama, Masjid al-Haram, ndio mkubwa
zaidi duniani ambao unazunguka sehemu takatifu ya Waislamu, inayojulikana kama,
the Kaaba.
Angalau watu 230 walijeruhiwa katika tukio hilo la aina yake.
Haijafahamika watu wangapi wameumia wakati winchi hilo lilipoangukia msikiti
huo.
Tukio hilo lilitokea majira ya saa 11:23 za jioni kwa saa za hapa
jana Ijumaa.
Picha za video zilizotumwa mtandaoni zinaonesha sehemu ikianguka,
huku sauti za watu waliochanganyikiwa zikitoaka, miili na damu zikionekana
katika sakafu ya eneo la msikiti huo.
Kiongozi wa mambo ya ndani ya nchi hiyo, Lt Sulayman Bin-Abdullah
al-Amr, alisema uchunguzi unafanyika ili kujua madhara ya tukio hilo, na "usalama
uliokuwepo katika maeneo haya.”
Essam al-Ghalib, mwandishi wa Jeddah, alisema winchi hilo
lilianguka na kuvunja kipande cha seminti chenye uzito mkubwa na kuwaagukia watu
ambao ama walikuwa wakisali au kutembelea katika eneo hilo.
Mecca kwa sasa inajiandaa kupokea maujaji kwa ajili ya hija ya
kila mwaka, ambapo hadi watu milioni mbili wanatarajiwa kuwasili katika jiji
hilo la Saudi kutoka duniani kote mwezi huu.
Taarifa zingine zinasema kuwa msikiti huo mkubwa kwa sasa
umezungukwa na winchi 15 kubwa kwa ajili ya kazi ya ukarabati inayoendelea
katika eneo hilo.
"Saudi Arabia inatakiwa kufikiri tena kuhusu usalama wa hatua
za usalama katika eneo hilo, “alisema,
ambapo eneo hilo lilikuwa na watu kama 800,000 katika msikiti wakati ajali hiyo
inatokea.
No comments:
Post a Comment