NAIROBI,
Kenya
WAVAMIZI
nchini Kenya walikata baadhi ya viungo vya mtu mwenye ulemavu wa ngozi
ili kwenda kuviuza kwa wachawi, ambapo taarifa zilisema kuwa, hatua hiyo imezua hofu ikihofiwa kuwa, huku ikidaiwa kuwa shambulio
hilo limefanywa na watu kutoka nchi jirani ya Tanzania.
"Watu
watatu walivamia nyumba yangu na kutaka pesa, “alisema mtu huyo albino mwenye
umri wa miaka 56 aliyejitambulisha kwa jina la Enock Jamenya, kutoka Magharibi
ya Kenya katika wilaya ya Vihiga. "Nilipowaambia kuwa sina pesa,
waliniomba sikio au mkono ili wakauze Tanzania.”
Wavamizi
hao walikata sikio, mkono, shingo na vidole, gazeti la Daily Nation liliripoti,
lakini baadae watu hao walikimbia, wakimuacha Jamenya akiwa amepoteza fahamu
na akiwa na majeraha kibao.
"Mmoja
wa watoto wake alikuja asubuhi kumuangalia baba yake, ambapo alimkuta akiwa
amelala chini katika dimbwi la damu,”alisema kaka yake Nixon Muhole
alipozungumza na gazeti la The Standard.
Katika
nchi ya jirani ya Tanzania, baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakituhumiwa kununua
sehemu ya viungo vya albino kwa ajili ya imani za kishirikina.
Vikundi
vya haki za binadamu vimeonya kuwepo kwa hatari ya ongezeko uvamizi wa watu
wenye ualbinism nchini Tanzania kutokana na kampeni za Uchaguzi Mkuu utakaofanyika
Oktoba 25.
Mtunga
sheria Isaac Mwaura, ambaye ana ualbinism, aliendelea kuonya kuwa wavamizi
wamekuwa wakivamia Kenya kwa ajili ya kufanya biashara nchini Tanzania.
Karibu
watu 76 wenye ualbino nchini Tanzania wameuawa tangu mwaka 2000, ambapo sehemu
ta viungo vyao vimekuwa vikiuzwa karibu dola za Marekani 600 (euro 528) na ambapo
mwili mzima unauzwa kiasi cha dola za Marekani 75,000, kwa mujibu wa wataalam
wa Umoja wa Mataifa (UN).
Taarifa
hiyo iliendelea kueleza kuwa watu kadhaa walionusurika wamebaki bilaya viungo
vyao baada ya kukatwa na kuchukuliwa na wavamizi hao.
Vikundi
vya haki za albino vilisema kuwa vinahofia wavamizi wanaweza kuilenga Kenya
baada ya serikali ya Tanzania kutoa taarifa kali kwa umma kukomesha vitendo
hivyo vya kikatili.
"Tunataka
serikali kuchukua hatua kali kuhusu vitendo hivi, kwa sababu vinatiashia maisha
yetu," alisema Martin Wanyonyi, kutoka taasisi ya kuwawezesha watu wenye Albinism.
No comments:
Post a Comment