Na Mwandishi Wetu
WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi), Celina Kombani (pichani), amefariki dunia jana akiwa
nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu.
Taarifa iliyotolewa jana na Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilillah na
baadhi ya wabunge waliozungumza jana, walisema Waziri Kombani alikuwa
akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu.
Kwa mujibu wa Katibu huyo wa Bunge, Kombani
alikuwa akisumbuliwa na magonjwa hayo kwa muda mrefu na kwamba mwili wake
utarejeshwa nchini kesho.
Kashilillah
alisema Bunge pamoja na Serikali kwa kushirikiana na familia ya marehemu
wanafanya taratibu za mazishi.
Hadi kifo
chake, Waziri Kombani alikuwa ni Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mashariki mkoani
Morogro kwa tiketi ya CCM na pia alikuwa ndiye mgombea wa chama hicho katika
jimbo hilo kwa uchaguzi wa mwaka huu.
Pamoja na kuwa Waziri katika Ofisi ya Rais (Utumishi), Kombani aliwahi
kutumikia wizara mbalimbali ikiwemo ya Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na pia Waziri wa Katiba na
Sheria.
No comments:
Post a Comment