BEIJING, China
OFISA Usalama wazamani wa China Zhou Yongkang amefungwa jela
maisha ikiwa ni mwanasiasa mkubwa kabisa kushitakiwa kwa kosa la rushwa chini
ya sheria ya Kikoministi.
Alipatikana na hatia ya rushwa, kukiuka taratibu na "kutoa
siri za nchi nje ya nchi ", Shirika la Habari la China la Xinhua liliripoti.
Hadi anastaafu mwaka 2012, Zhou alikuwa mmoja wa watu wenye nguvu
sana nchini China.
Na mwaka mmoja baadae alikuwa akichunguzwa kama mpango kabambe wa
kupambana na rushwa wa rais Xi Jinping.
TV ya serikali ilionesha picha ya Zhou, 72, akikubali kosa katika
shitaka lililoendeshwa `incamera’ kaskazini ya
jiji la Tianjin.
Wakati akimjibu jaji, alisema hajakata rufaa.
"Nimebaini nimekiathiri chama na Watu wa China. Nakili na
kujutia makosa," alisema.
No comments:
Post a Comment