MADRID, Hispania
KLABU ya Real Madrid imethibitisha kuwa, imemchukua Rafael Benitez
kama kocha wao mpya kwa mktaba wa miaka mitatu.
Kocha huyo Mhispania mwenye uzoefu mkubwa katika soka alikuwa
akipewa nafasi kubwa ya kuchukua mikoba iliyoachwa wazi na Carlo Ancelotti wakati
alipoachana na Real wiki iliyopita.
Kutangazwa kwa Benitez kumeiacha Napoli inayoshiriki Ligi ya Serie
bila kocha baada ya Benitez kumalizana nao mwishoni mwa msimu na sasa atakuwa
na kibarua cha kuiongoza Real kufanikiwa katika La liga na Ligi ya Mabingwa wa
Ulaya.
Benitez ambaye ni kocha wazamani wa Real Madrid, aliiongoza Valencia
kutwaa mataji mawili ya Hispania kabla ya kuifundisha Liverpool kwa miaka sita
na kuiwezesha kufanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya mwaka 2005.
Kocha huyo alikwenda kuifundisha Inter na Chelsea, wakishinda
mataji ya Ligi ya Ulaya na baadae aliiongoza Napoli kutwaa taji la Coppa Italia
miezi 12 iliyopita katka kampeni yake ya kwanza kwenye uwanja wa Stadio San
Paolo.
Real Madrid ilimaliza ya pili katika La Liga nyuma ya Barcelona
msimu huu na kupoteza mchezo dhidi ya Juventus katika nusu fainali ya Ligi ya
Mabingwa wa Ulaya.
No comments:
Post a Comment