NA Mwandishi Wetu, Tanga
MABINGWA wa Ligi kuu soka Tanzania bara
mwaka 1988,Coastal Union,Wagosi wa Kaya imeingia mkataba wa miaka miwili na
aliyekuwa Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Jackson Mayanja ambaye ni
raia wa Uganda kuifundisha timu ya Coastal Union katika msimu ujao wa
Ligi kuu soka Tanzania Bara itakayoanza Mwezi Agosti mwaka huu.
Utiliaji wa saini wa Kocha huyo
ulifanyika (leo)jana mjini hapa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa timu
ya Coastal Union akiwemo Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Albert Peter na Katibu
Mkuu wa timu hiyo,Kassim El Siagi.
Akizungumza baada ya kumalizika zoezi
hilo,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema kuwa kutokana na
umahiri aliokuwa nao kocha huyo wanaimani kubwa ataipa mafanikio timu hiyo hasa
katika harakati za kuhakikisha inafanya vizuri ligi kuu msimu ujao.
Amesema kuwa uwezo wa Kocha huyo
utaleta matumaini makubwa ya mafanikio hasa ukizingatia ni kocha mwenye uwezo
mzuri wa kufundisha na kuzipa mafanikio timu hivyo tunaamini kuja wake kwetu
itakuwa chachu katika maendeleo.
Mayanja ambaye aliwahi kuzifundisha
timu za soka Kiyuvu FC ya Rwanda,Timu ya Mamlaka ya Mapato nchini Uganda
(URA),Vipers FC ya
Bunamwaya na KCC ya
Uganda amesema kutua kwenye timu hiyo kumpa faraja kubwa hivyo atahakikisha
anatoa mchango wake kwenye kuipa mafanikio.
Amesema kuwa mipango yake mikubwa ni
kuhakikisha timu hiyo inang’ara
katika michuano ya Ligi kuu msimu ujao ikiwemo kubadili aina ya mchezo wa timu
hiyo ili iweze kupata mafanikio kwa kuweka umoja baina ya wachezaji mashabiki,
wanachama na wapenzi.
Amesistiza pia umuhimu wa mshikamano
baina ya wapenzi,wanachama na viongozi ili kuiwezesha timu hiyo kuchukua
Ubingwa wa Ligi kuu msimu ujao kwani dhamira yake ni kutaka kuona timu hiyo
inang’ara kwenye
medani za kitaifa na kimataifa.
No comments:
Post a Comment