MANCHESTER, England
KLABU ya Manchester City hadi sasa imewasilisha maombi mara mbili
huku lile la mwisho likiwa linakaribia kiasi cha pauni Milioni 40. Yote
yametupiliwa mbali na Liverpool.
Imebainishwa kuwa Liverpool hawataki kumuuza mchezaji wao Raheem
Sterling mwenye umri wa miaka 20 chini ya kiasi cha pauni Milioni 50.
Chanzo kilichokaribu na klabu hiyo ya Merseyside imedokeza kuwa
Man City haina mpango wa kukubali kumuachia mchezaji huyo endapo Man City
hawataongeza pauni Milioni 10 ndipo wataweza kumuachia.
Man City pia wanajua kuwa klabu zingine kibao nazo zinamtaka
mchezaji huyo ikiwemo Real Madrid ya Rafa Benitez, Arsenal na Chelsea.
Hawataki kabisa kumkosa Sterling
na wanatarajia siku chache sijazo wanatarajia kuwasilisha ofa ambayo
itawaridhisha Liverpool.
Man City pia wako tayari kuijaribu Arsenal kumnunua mwenzake na Sterling wanaecheza naye timu ya taifa ya England Jack Wilshere.
Hatahivyo, kocha wa Gunners Arsene Wenger anasisitiza kuwa shujaa
huyo wa England aliyefunga mabao mawili wakati England ikiibuka na ushindi wa
mabao 3-2 katika mchezo wa kufuzu kwa fainali za
Mataifa ya Ulaya huko Slovenia Jumapili ya wiki iliyopita hauzwi.
No comments:
Post a Comment