Tuesday, 9 June 2015

Ufungaji mashindano ya 54 ya taifa ya riadha ulivyofana

Baadhi ya wanariadha wa mbio za mita 1500 wakishindana katika mashindano ya taifa mwishoni mwa wiki katika viwanja vya shule ya Filbert Bayi Mkuza Kibaha.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akiteta na watoto waliokuwa wakibeba medali na fedha kwa ajili ya washndi wa mashindano ya 54 ya riadha ya taifa.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Halima Kihemba (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa shule za Filbert Bayi, Anna Bayi wakati wa mashindano ya taifa ya riadha.

 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akiwa na timu ya Kaskazini Unguja baada ya kumalizika mashindano ya taifa ya riadha mjini Kibaha.
Makamu wa Pili waRais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akiwa katika picha ya pamoja na timu ya mkoa wa Singida wakati wa mashindano ya taifa ya riadha.


Makamu wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,  Balozi Seif Ali Idd akiwa na mabingwa wa riadha wa Tanzania timu ya Mkoa wa Mjini Magharibi baada ya kumalizika mashindano ya taifa 2015 Kibaha mkoani Pwani.
Mkurugenzi wa mashindano ya 54 ya taifa ya riadha yaliyofanyika kwenye viwanja vya shule za Filbert Bayi, Filbert Bayi akitangaza matokeo ya mashindano hayo.

Makamu wa Rais wa Zanzinbar Balozi seif Ali Idd (kushoto) akiangalia tracksuit alilopewa na Katibu Mkuu wa Riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui wakati wa mashindano ya taifa ya riadha yaliyofanyika kwenye viwanja vya Filbert Bayi Mkuza Kibaha mkoani Pwani.
Wariadha wazamani wa Tanzania, Meta Petro (kushoto) na Francis John ambaye ni kocha wa timu ya taifa na meneja wa mashindano ya taifa ya 54 ya riadha yaliyofanyika Mkuza Kibaha.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia akizungumza wakati wa ufungaji wa mashindano ya 54 ya taifa ya riadha kwenye viwanja vya shule za Filbert Bayi.

No comments:

Post a Comment