Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imemtaka
mwakilishi wa miss Tanzania kwenda kuitendea haki lugha ya Kiswahili katika
mashindano ya miss word yaliyopangwa kufanyika China Desemba nane mwaka huu.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo,
Dk Harrison Mwakyembe wakati akimkabidhi bendera ya taifa Miss Tanzania, Queen
Elizabeth (pichani), anayetarajia kuondoka Novemba 8 kwenda Sanya, China, ambako shindano
hilo litafanyika.
Akizungumza Waziri
Mwakyembe alisema Serikali kupitia Wizara yake haikabidhi bendera hovyo hovyo
isipokuwa unapokabidhiwa lazima ukalitendee haki taifa lako.
Alisema kutokana na
hilo, Queen Elizabeth anapaswa kwenda kufanya vizuri katika shindano hilo kubwa,
ambalo litasaidia kuitangaza Tanzania vizuri kama tu atakitumia vizuri
kiswahili katika mashindano hayo.
Mratibu wa shindano la Miss Tanzania na Mkurugenzi wa The Look Company, Bi. Basila Mwanukuzi. |
Alisema kiswahili ni
moja ya lugha kubwa duniani, kwa hiyo anapaswa kuitangaza kwenye mashindano
hayo.
Mbali na hilo
aliipongeza kampuni ya The Look, ambao
ni waandaaji wa mashindano hayo kwa kurejesha heshima ya Miss Tanzania
na kuahidi kuboresha zaidi huku akiwasisitizia kuwa warembo wote wanaoshiriki
shindano hilo watapata nafasi ya kufanyakazi katika Shirika la Ndege Tanzania,
ATCL, na mashirika mengine, ambayo yatakuwa yatakuwa tayari kuwasaidia.
Wao kama Serikali
wanaamini katika shindano hilo mrembo huyo atafanya vizuri na kuipeperusha
vema.bendera ya nchi.
Naye Elizabeth alisema
anakwenda China kushindana na si kushiriki kwa hiyo Watanzania wategemee mambo
makubwa kutoka kwake.
Alisema amejiandaa
vizuri na shindano hilo na anaimani katika mashindano hayo atafanya vizuri ili
kuitangaza nchi yake.
Kwa upande wa muandaa wa
shindano la Miss Tanzania, Basila
Mwanukuzi alisema Elizabeth amefanya maandalizi ya kutosha ambayo kamati yake
imejirisha kuwa anakwenda kushindana na so kushiriki.
Alisema kurejea kwa Miss
Tanzania ambayo inasaidiwa na wadau wengi, kumelifanya shindano hilo lirudishe
heshima yake kama ilivyokuwa awali.
Alisema anawashukuru
wadhamini waliojitikeza kufanikisha, huku akiendelea kuomba wadhamini wengine
wajitokeze zaidi kuwapiga jeki.
No comments:
Post a Comment